Tuesday, November 23, 2010

AIRTEL ONE8 KUSAIDIA SHULE BAGAMOYO KUPITIA WIMBO WAKE UNAOTAMBA



KAMPUNI ya simu za Mkononi Airtel watautumia wimbo wa 'Hands across the World' ulioimbwa na wanamuziki mbalimbali wa kimataifa akiwemo Ali Kiba pamoja na wanamuziki wengine saba akiwemo R Kell kujengea shule ya msingi ya Kiromo


Akizungumza Dar es Salaam leo, Mkurgenzi mtendaji wa Airtel nchini Sam Elangalloor alisema wimbo huo utachangia ujenzi wa shule hiyo kupitia mlio wa simu wa one kupitia mtandao wa Airtel live port au kutumia ujumbe wenye neno ONE8 kwenda 6262 ambapo pesa atakayokatwa mteja huyo itaingia moja kwa moja katika ujenzi wa shule hiyo



Alisema Airtel pia itaendela na mradi huo wa kusaidia shule zaidi ya 50 kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na kwamba na kwamba mradi huo wa kujendga shule ya Kiromo unatarajia kumalizika Machi mwakani


Kwa upande wake Ali kiba alisema wimbo huo umeweza kumpatia manufaa makubwa ikiwemo kufanya kazi pamoja na wasanii wa kubwa akiwemo msanii wa kimataifa R Kelly, Afrika 2face (Nigeria), Amani (Kenya), Movaizhalene (Gabon), JK (Zambia), Fally Ipupa (Kongo) na Navio (Uganda).

Alisema kundi hilo la ONE8 litatengeneza albam ya pamoja itakayokuwa na jumla ya nyimbo 12 ambapo katika albamu hiyo kila msanii atapata nafasi ya kutunga wimbo wake mmoja.





burudan mwanzo mwisho

No comments:

Post a Comment