Tuesday, November 23, 2010

Tamasha kubwa la Miaka 6 ya MITIKISIKO YA PWANI kufanyika Diamond Jubilee, Dec 3...!


Mwaka jana Mitikisiko ya Pwani ilifanyika kwenye ukumbi wa PTA Sabasaba na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya watu tokea pande zote za jiji, safari hii mambo yatafanyika Diamond Jubilee katika ukumbi mkubwa wa burudani jijini Dsm



Zawadi kadhaa zitatolewa kwenye Tamasha hilo ikiwa pamoja na zawadi kutoka kwa wadhamini wetu, oryx wauzaji wa mafuta, gesi na majiko ya gesi nchini pamoja na fedha taslimu ambazo zitachukuliwa na wapenzi wa Taarabu huku watu mia moja wa kwanza watajipatia t-shirts.


Mpaka sasa ni bendi tisa ambazo zimethibitisha kushiriki katika tamasha hilo ambalo litafanyika 03/12/2010 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee huku likimshirikisha msanii mkongwe wa Taarabu, Bi kitude ambaye pia mbali na kutumbuiza atakabidhiwa Tuzo ya Heshima kulingana na Mchango wake wa muziki kwa muda mrefu. Bendi hizo ni pamoja na:

1) Coastal Modern Taarab
2) Dar Modern Taarab
3) East African Melody
4) Five Star Modern Taarab
5) Jahazi Modern Taarab
6) New Zanzibar Modern Taarab
7) Super Shine Modern Taarab
8) Tandale Modern Taarab
9) TOT Taarab


Wadhamini wa Tamasha hilo ni ORYX, wauzaji wa mafuta, gesi na majiko ya gesi nchini, Tigo, Regency Hotel, PSI, ICV Security Company, Malaika Beach Resort, Zizou Fashion, Dida classic boutique, Jolyety Saloon.

No comments:

Post a Comment