Friday, November 19, 2010

Raisi JK afungua bunge jipya la 10, asisitiza kushughulikia maslahi ya wasanii...!

Mheshimiwa Raisi Jakaya Kikwete akilihutubia bunge jipya tukufu la Jamhuri ya Tanzania, na kufungua rasmi shughuli zake mbele ya wabunge na wakuu wengine wa nchi, mabalozi na wageni wakimataifa na kitaifa jana jijini Dodoma
Pamoja na mengi mazuri aliyoainisha ktk hotuba yake hio, amesisitiza kushughulikia maslahi ya wasanii wa Bongo ( wa muziki na filamu) pia akiwakumbusha wabunge kuwa huko Duniani kwa wenzetu wasanii ni moja ya watu tajiri sana tofauti na hapa kwetu....

"Katika kipindi hiki pia tumeshuhudia maendeleo makubwa ya sanaa za maonyesho yaani muziki na filamu. Wameibuka wanamuziki wengi wazuri wa muziki wa kizazi kipya, taarabu na rumba.
Pia kuna maendeleo makubwa ya filamu na uigizaji. Kuna haja ya kujipanga vizuri kusaidia kuendeleza sanaa hizo na wasanii wake.
Mimi binafsi nimeanza kuchukua hatua za hapa na pale za kujaribu kutatua baadhi ya matatizo yanayowakabili. "
"Sasa wakati umefika wa kuwa na mipango thabiti ya kuendeleza fani hizi na kuwawezesha wasanii kuendeleza vipaji vyao na kunufaika na kazi zao."


No comments:

Post a Comment