Thursday, January 6, 2011

Tumeanza mwaka vibaya, tukiendelea hivi tutapotea, tujikumbushe chanzo cha machafuko ya jirani zetu...!


Viongozi wa juu wa CHADEMA, wakiongowa na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe (Watano kulia) na katibu mku, Dk.Wilbroad Slaa(Wasita kulia) wakiongoza maandamano yaliopigwa marufuku na polisi jana mjini Arusha.Hatimaye polisi iliwatolea uvivu na kuwapiga kwa mabomu ya machozi. Habari zaidi zaeleza kuwa Mbowe anashikiliwa na polisi.


Maandamano yakiwa yamepigwa stop



Mke wa Katibu Mkuu wa Chama cha CHADEMA Dk.Wilbroad Slaa, Josephine akiwa ametapakaa damu baada ya kujeruhiwa vibaya kwa kipigo na polisi wakati wakivunja maandamano ya viongozi na wanachama wa chama hicho yaliyofanyika mjini Arusha jana.Katika maandamano hayo watu kadhaa walijeruhiwa baada ya kupigwa na pilisi wa kutuliza ghasia.Picha kwa

(chanzo cha habari http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/100142-maandamano-ya-chadema-arusha-mabomu-yarindima-28.html)

Taarifa mpya zilizopatikana zinasema watu 10 wameripotiwa kuuawa ktk mji huo wa Arusha kwenye majibizano baina ya Polisi na wafuasi wa CHADEMA

Kwa mujibu wa Shirika la utangazaji la Uingereza BBC ghasia zilianza baada ya polisi kumkamata mwenyekiti wa kitaifa wa chama hicho cha CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe na mbunge wa Arusha Mjini Bw. Godbless Lema wakiwa wanaelekea kuhutubia mkutano wa kisiasa. Baadae polisi walimkamata aliyekuwa mgombea wa chama hicho cha CHADEMA kwenye uchaguzi wa Uraisi uliofanyika Oktoba 201, Dk. Wilbroad Slaa.
(Habari kutoka gazeti la jioni la Dar Leo 6/1/2011)

No comments:

Post a Comment