Wednesday, March 16, 2011

Umaarufu wa makalio wamsababishia kifo msanii chipukizi wa Hiphop...!


Claudia Aderotimi msanii wa kike wa hiphop anayetokea nchini Ghana amefariki baada ya kupata matatizo kutokana na ndoto zake za kuongeza makalio ili awe maarufu kama kina J-Lo na Nick Minaj pichani.

Claudia (20 yrs) alipanda ndege mpaka Marekani akitokea London anakopiga kitabu kwa lengo hilo la kufanyiwa upasuaji wa makalio akiamini kuwa akiwa na BIG BOOTY atakuwa maarufu zaidi km ilivyo kwa Nick Minaj. Rafiki yake wa kike ameeleza kuwa alipata matatizo ya kupumua masaa 12 baada ya kufanyiwa upasuaji huo na kufariki dunia baadae kidogo.

No comments:

Post a Comment