WASANII wa muziki wa kizazi kipya wanaotamba na sauti tamu ktk nyimbo zao na wenye uwezo mkubwa jukwaani kwa muziki wa ‘Live’ Ali Kiba na Elias Barnaba maaarufu Barnabas wanatarajia kutumbuiza katika jukwaa moja na bendi ya muziki wa dansi iliyojizolea umaarufu mkubwa nchini Mapacha watatu.
Mmoja wa wakurugenzi wa mapacha watatu Kharidi Chokoraa maarufu Tora bora amesema Onyesho hilo la pamoja litafanyika Jumapili Julai tatu katika Ukumbi wa Mzalendo Pub Kijitonyama.
Chokoraa amesema lengo la burudani hiyo ni kuwapa ladha tofauti mashabiki wa Mapacha watatu na huenda ikafanyika kila Jumapili ya kwanza ya kila mwezi ili kudhihirisha kwa mashabiki ujio wao wa kutoa burudani hasa katika kiunga cha Mzalendo.
Amesema maandalizi yote yamekamilika nawasanii hao watapiga live na bendi hiyo hivyo mashabiki watarajie kupata burudani ambayo hawajawahi kuipata kutoka kwa wasanii wa ndani.
“unajua Ali Kiba ni msanii mkubwa na ni mkali jukwaani na pia Barnaba ambaye amewahi kuimba na Faly Ipupa alipokuja nchini na mapacha watatu ndo usiseme.” Alisema Chokoraa.
Ali kiba amewahi kutamba na nyimbo kama cinderela,mac Mugan,Karim na sasa anatamba na kibao cha Mapenzi yana run Dunia ambacho kimejizolea umaaarufu mkubwa wakati Barnaba ametamba na vibaon kama Njia panda na mbalamwezi na nyingine nyingi.
No comments:
Post a Comment