
Show zilianzishwa na wasanii mbalimbali kutumbuiza, wengine wakashangiliwa na wengine kuzomewa kwa Sauti kubwa ya umati, ktk walioshangiliwa na kuzomewa wapo wasanii wawili zaidi Bushoke na Izzo B ambao makelele waliyopigiwa yana maana kubwa sana na hayatakiwi kupuuzwa kabisa!
Bushoke alizomewa sana pale alipoanza kuifagilia serikali eti imefanya mambo mazuri mengi sana, umati mkubwa wa vijana ukapinga ktk staili hio
Izzo B ndie aliyeshangiliwa sana zaidi alipoimba kile kibao chake cha "RIZ ONE Ongea na Msure" nyimbo inayomwelekeza Riz aongee na mkubwa juu ya mambo ya serikali ambayo mengi hayajakaa sawa! pia alipotaka umati uzomee TANESCO, umati ulizomea saaaaana!
dancers wa DiamondShow ilikuwa kali sana, wapenzi waliohudhuria walilithika ile mbaya..... waandaaji wa Fiesta, Clouds Media walithamini mchango wa wasanii na wadau kibao waliotoa mchango wao tangu mwanzoni mwa utamaduni huu ambao umefikia miaka 10 sasa, Tuzo na heshima zilitolewa kwa wasanii.
BiGuPP sana Wazee wa FiEsTaa!
kuelezea ile show nahisi maneno hayatatosha, zaidi tembelea photos kunako TeenTz.com



No comments:
Post a Comment