Friday, September 30, 2011

MAKAVULIVE kupagawisha ndani ya MASAI CLUB ILALA, Jumamosi ya Kesho...!


Kundi la Makavulive litavamia ktk club ya disko ya MASAI Club pande za ILALA kesho jumamosi 1/10/2011 na kutoa show kali kwa fans wataohudhuria pale kati.
Likiongozwa na OMMY G, majamaa wameahidi kutoa burudani ya uhakika usiku huo ambapo show itatanguliwa na disko kali kutoka kwa Dj Niko Track aka SharpShooter!

Makavu wataperform nyimbo zao zote zilizowahi kutoka kitambo na hizi mpya ikiwemo "Mambo mambo" waliyotoka kuiachia hivi karibuni.

Makavulive linaundwa na wasanii kama Dullayo, Ommy G, Xdizo, Mon G, Eazy Dogg, Pompin na Joslin.........

Wednesday, September 28, 2011

G Mabovu, Bac-T Kusindikiza uzinduzi wa IWACU ya JAY-POLLY, nchini RWANDA.....!

Msanii maarufu nchini Rwanda Jay-Polly ambaye ni member wa kundi linalo julikana kama Tuff Gang, anatarajia ku launch album yake tarehe 07/ October/ 2011, Album hii itakuwa ya kwanza kwa msanii huyo, na ita sindikizwa na wasanii wengine wa nyumbani kama vile Diplomat, Pacson, Bac-T, Paccy, MC Mande, Kamichi, Tom Clouse, Uncle Austin, Sandra miraji, Just Family, Dream Boyz na wengine wengi.

Na pia kutakuwa na wasanii kutoka nje ya Rwanda kama vile T-Max kutoka Burundi na Geez Mabovu kutoka Tanzania

Burundian Rapper: T-Max

Tanzanian rapper: Geez mabovu

Source; Up In KGL


MISS UTALII DODOMA 2011/2012 KUSHUDIWA NA WABUNGE, WAKUU WA WILAYA NA MKUU WA MKOA DODOMA

Waheshimiwa wabunge wote wa Majimbo ya mkoa wa Dodoma, wakuu wa Wilaya zote na mkuu wa mkoa wa Dodoma, ni miongoni mwa wageni mashuhuri walio alikwa kuhudhuria shindano la kumpata mrembo wa utalii wa mkoa wa Dodoma 22-10-2011. Shindano hilo limepangwa kufanyika katika ukumbi wa hoteli ya kitalii ya New Dodoma hoteli, na kushirikisha jumla ya warembo kumi na tano toka wilaya zote za mkoa wa Dodoma, ambao hivi sasa wana endelea na kambi ya mazoezi katika Hoteli hiyo ya New Dodoma Hotel chini ya mkufunzi wao Neema Isdory (Miss Utalii Njombe 2010/2011) na Tabia Msuta (Miss Utalii Vyuo Vikuu Kanda ya Kati 2010/2011.
Miss Tourism Tanzania Symbol Of National Heritage - Do Value Added Pageant
"Lets Visit & Promote Tanzania National Parks -Tourism is Life ,Culture is Lining"
Regards,

Gideon E.G. Chipungahelo
PRESIDENT / C.E.O
Hotline: + 255 - 715/754/773 - 318 278.

New Song; Raz Q ft. Fonabeez - BORN 2 SHINE

Track : BORN TO SHINE
Artist : RAZ Q FT FONABO ( FONABEEZ )
Studio : TUFF RECORDS MOROGORO
Prod. : GQ
Location : MOROGORO
Contact : 0714625481 - RAZ Q

: 0657659969 - GQ
I would like to hear your comment concerning this song
please revert through this E-mail
i appreciate both sides of your comments
Thanks.
GQ

LISTEN & DOWNLOAD FROM MAKAVULIVE PLAYLIST HAPO JUU

FOR PROMO ONLY

Wakazi - HIGHER

Tuesday, September 27, 2011

BARUA YA WAZI KWA DICOTA - ALBINO FULANI

DICOTA officials,

I would like to commend your efforts on putting together the event to mark 50 years of Tanzania’s Independence. In this day and age where our country is going through various crises including severe corruption, water and energy deficiencies, poor standards of living, leadership and political conflicts and so forth; we need a new and improved system. I therefore strongly support your network effort linking fellow Tanzanians living in the US to the ones back in Tanzania.

I was happy; yet, saddened to see that DICOTA is hosting and possibly paying for a Kilimanjaro Band (Wananjenje), Jahazi Modern Taarab and King Kiki for music entertainment at the event and disregarding the fact that there are Tanzanian artists in the diaspora community. We have mainstream and non-mainstream Tanzanian artist living in the USA. The general expectation would be to involve and support these artists, whose works are hereby showcased and incorporated into today’s entertainment and culture.

Not to challenge or downplay your current guest musicians, but the list could have been more diversified to entertain more guests. It is vital to consider all groups. Higher number of viewers and listeners enables Bongo Flava to get more airtime compared to any other gene in all Swahili based radio or TV stations all over the world. Surprisingly, Bongo Flava artists were not included in your list.

Most will argue that in the 21st century the world is moving in a very fast economic and social pace. Instead of old-fashioned, traditional mentalities and stagnant ideologies, the community could benefit more from innovative, diverse leadership. We need to keep up.

This kind of leadership is what we are trying to change in Tanzania. Most will agree that this is the type of leadership that only focuses on self-interest and personal gain. It should be remembered that one key campaign strategy for CCM and JK’s presidential campaign (the ruling party and current president) was to campaign with the kind of artists DICOTA left out.

By ignoring these talented artists who have been representing the Republic of Tanzania by taking part in cultural festivities amongst other events in the United States; it’s fair to question the blatant discrimination against fellow musicians and lack of diversity or acknowledgement of the hard work of community members. Based on the upcoming event, DICOTA has demonstrated a lack of insight as to what transpires between Tanzanians living in the US and those back in Tanzania.

I recommend that, prior to assuming leadership duties as members of the diaspora community; DICOTA officials should meet and exceed a minimum qualification of frequently visiting the country they are representing to update their knowledge of the current situation rather than depending on Michuzi and other blogs. Today, it’s about inviting music artists but tomorrow might be choosing a president.

Albino Fulani

Friday, September 23, 2011

Chinua ACHEBE Amkomalia 50 Cent mpaka amebadili Jina la Movie yake!!

Mwandishi Legendari wa vitabu Afrika CHINUA ACHEBE alimlazimisha Rapa maarufu wa Marekani 50 Cent kubadilisha jina alilotaka kutumia ktk filamu yake mpya "Things Fall Apart" ambalo ni jina la riwaya ya Mzee huyo, jina la riwaya ya Chinua Achebe limebamba mno kiasi cha kusomwa na kuuza zaidi ya nakala milioni 8 duniani kote.

Chinua Achebe baada ya kusikia juu wa ujio huo wa filamu ya Cent, timu yake ya kisheria ilimvaa mnyamwezi 50 Cent na jamaa akataka kama kulipa $ 1,000,000 ambazo Chinua Achebe alikataa na kuona kama anatukanwa!


Sasa 50 Cent amebadili jina la filamu hio na kuiita "ALL THINGS FALL APART" movie inayoelezea maisha juu ya mchezaji wa mpira wa miguu ambao ni kukutwa na kansa kisha mambo yote yanamwendea mrama.

New Video; NAS B - "DUA LA KUKU"

MO RACKA FT JUX - KAMA CHANGU NTAPATA

Nyimbo mpya; Jide ft. Tuku - Mimi ni mimi (Iam who iam)



10 years ago I met someone who changed my life musically. I continued following his footsteps working hard listening to the advice he gave me every time we chatted. All this time I had a dream to do a song with him but didn’t know when exactly its gonna happen but I still believed one day this dream will come true. Fast forward to 2011, By the grace of God i am who i am, God made my dream come true, the this collabo with the legendary African musician Oliver "Tuku" Mtukudzi from Zimbabwe.
Thanks for the support and enjoy the music!!!

Kuusikiliza wimbo wa MIMI NI MIMI - Jide Feat Mtukudzi bonyeza link hapo chini

AY kuitoa kimasomaso Bongofleva....!

Baada ya kufanikiwa kupiga bonge la collable na mwadada La myia na Romeo "Speak with ur body" sasa kinachofata ni kufanya tour na mwanadada inayoitwa No limit katika nchi mbali mbali duniani, akiwa na wasanii wengine wakubwa kutoka marekani kama Gicci maine na wengine kibao. kwa sasa AY anakamilisha collable yake nyingine na msanii mwigine kutoka marekani T Pain.

from; DjFetty Blogspot

Monday, September 19, 2011

SILVER aachia VIDEO ya wimbo Mpya kabisa...."WAWEZA KWENDA "

Msanii wa Hiphop Bongo SILVER ameachia Video ya wimbo wake mpya "WAWEZA KWENDA" alioshirikiana na STEVE RnB, akiwa amefanya tofauti na wasanii wengi walivyo na kawaida ya kuanza na Audio kabla ya kuachia Video za nyimbo hiyo.


SILVER ameachia Video ya nyimbo hio huku tayari ana nyimbo nyingine aliyoachia redioni siku chache zilizopita na inaendelea kufanya vizuri sehem mbalimbali. Nyimbo hio inaitwa "BONGO TZ" ambapo amemshirikisha Jay MOE wamefanyia Bongo Record chini ya P . Funk. Awali Silver alitoka na ngoma inayoitwa "NAFANYA" kwenye chorus akamshirikisha Steve RnB


Nyimbo Mpya; LINE YA SIMU by KIMBUNGA

Msanii wa Hiphop MwanaHarakati KIMBUNGA au KIM ameachia ngoma mpya inayokwenda kwa jina la LINE YA SIMU, ngoma imefanyikia mzuka records kwa Producer JC akiwa amewashirikisha abass kubaff na richie rich unaweza kui-download ktk Playlist ya Makavu hapo juu kwa ajili ya PrOmo tu!

Kabla ya hii KIMBUNGA alishaachia ngoma zingine kibao kwa mfululizo ikiwemo I AM A GENIOUS aliyofanya kwa LAMAR mwaka jana 2010.

Nyimbo mpya; Wakazi - 'A Million'


Another song from Mixtape Ya Ukweli Vol.2. MYU3 is comin out soon

Kuskiza na ku-download for free kabisa, nyimbo ya A MILLION kutoka kwa WAKAZI check hapo juu ktk Playlist ya Makavulie

Happy Birthday Dj CHOKA

Dj Choka aka Mr. Apitite
http://www.bongostarlink.com/

Friday, September 16, 2011

Soko la SIDO Mbeya lateketea kwa MOTO

Tukio lingine kubwa la ajali ktk mwenzi huu wa September limetokea leo jijini Mbeya, baada ya lile kubwa zaidi kutokea pande za Nungwi huko Zanzibar baada ya Meli kuzama. Soko kubwa la SIDO Mbeya limeungua





















Nimezipata hizi habari baada ya kuwasiliana na Mdau wangu mkubwa kutokea MBEYA, jamaa anaitwa Dj Fredy....... fuatilia chats zetu chache uone! Inasikitisha

Makavu; Niaje jembe langu?

Dj Fredy; poa kaka japo sio kwema huku soko limeungua balaa

Makavu; duh soko gan tena


Dj Fredy; soko la sido ambapo lilihamiha lile la mwanjelwa baada ya kuungua angalia kwenye group letu utaona picha


Makavu; poa, polen sana kaka
watu hawajawafa?


Dj Fredy; duh asante kaka hakuna mtu aliekufa kaka


Makavu; poa


Dj Fredy; bado kaka yaani sasa hivi eneo lote la manjelwa mpaka soweto ni kama kilomita moja hivi biasharazimefungwa ni balaaaaaaaa

Makavu; Zima moto vp hawajafika?

Dj Fredy; walikuwepo hapa wanacheza cheza tu kwanza wamekuja kwa kuchelewa sana

Makavu; Chanzo nini mzaz?

Dj Fredy; kaka mi nilikuwepo pale wakati moto unawaka kila mtu anaongea lake but kuna mashushushu nimewaweka pale soon nitawapa ukweli ulivyo

poa kaka natoka kidogo baadae kaka

Makavu; naskia hili sio soko la kwanza kuungua Mbeya?


Dj Fredy; aah kaka yameungua masoko matatu sasa na yote ni makubwa sana hapa mbeya kwa kweli kwa hili la sasa umaskini huu hapa nauona mbeya kaka





Picha zaidi BOFYA HAPA


Thursday, September 15, 2011

Join the Campagn, OKOA TANZANIA..........!

Mdau, Kuna kampeni ya kuchangia ununuaji wa LIFE JACKETS elfu kumi kuwasaidia wasafiri wa majini, ili kuepuka maafa kama yale yaliokwisha tokea......

Hawa ndugu walinusurika kwa kutumia Magodoro na Friji ambavyo sio kabisa utaratibu wa safari za vyombo vya majini. Hivyo zinahitajika Life Jacket na Maboya kibao yakutosha kuokoa ndugu wengi zaidi!


"Ask not what your country can do for you; ask what you can do for your country."

Tuesday, September 13, 2011

Nyimbo ya maombolezo "Njia yetu ni moja" - Darasa, Diamond, R.O.M.A & Young D

Wimbo huu ni maalumu kwa ajili ya wenzetu waliofikwa na misiba katika ajali ya MV Spice huko Zanzibar ambao kimsingi ni wetu sote watanzania,waafrika na ulimwengu mzima kwani sote tu sehemu ya ulimwengu mmoja.

Wasanii walioshiriki ni Diamond Platinumz,Darasa, Roma “Mkatoliki” na Young D

Producer ni Maneke ndani ya AM Records


Pia kuna wasanii wengi na nyimbo mbalimbali wanaendelea kuungana na WaTanzania wote ulimwenguni wakitoa mchango wao ktk kuwafariji wote walioguswa na JANGA hili la Taifa

Blog ya Makavu inawapongeza wote wanaoendelea kuonyesha moyo wao na Mungu Awabariki.

BongoCelebrity.

Monday, September 12, 2011

SAIDIA ZANZIBAR.......


Why We Do This How To Help Who We Are Where It Goes

On 10th September 2011, the ferry M.V. Spice Islander, travelling between Dar es Salaam, Zanzibar, Pemba and Tanga, capsized in deep waters in the Pemba Channel, north of Zanzibar island.

The true numbers of those injured or dead in the tragedy has yet to be established, but it is now acknowledged that there were many more passengers than the 610 listed on the ship manifest. As of Saturday night, 200 are dead, 500 have been rescued and many are still missing. The full extent of the tragedy will not be known for several more days.

Saidia Zanzibar is an emergency fundraising website, to allow caring members of the community, in Zanzibar and the world at large, to commit some of their time and money to assist those tragically affected by the disaster.

We will be posting updates in the coming days, as more information becomes available and as our efforts grow.

The fundraising effort is being overseen by a committee of volunteers drawn from the Zanzibari Business Community, dedicated to supporting the relief efforts and reaching out into the community to ensure that the money reaches its intended purpose.


We are currently accepting donations to the following bank account:-

Acc Name: SAIDIA ZANZIBAR
Federal Bank Of Middle East, Zanzibar Branch
Acc No: 037400 (the following currencies accepted: USD, GBP, Euro, Tsh)
Detail: FEDERAL BANK OF MIDDLE EAST
SWIFT 1: FBMETZTZ
SWIFT 2 :BKTRUS33 (Correspondent Bank)

Our account is monitored by the Committee, one of whom is an auditor, is open to public scrutiny upon request, and is co-signed by five members of the committee, drawn from the Zanzibari business community.

Any queries regarding this account and our banking procedures should be sent to saidia@saidiazanzibar.org.

We are also accepting donations of clothing and sheets to our drop-off point at the ZATI Office, 1st Floor, Cine Afrique, Malindi, Stone Town, Zanzibar.

Video Mpya; DULLAYO - MIDA YA KAZI

Sunday, September 11, 2011

SIKU TATU ZA MAOMBOLEZO........ SUMATRA hawawajibiki ipasavyo kukagua usafiri...!


KUFUATIA msiba mkubwa uliotokana na ajali ya kuzama kwa meli ya Spice Islander katika bahari ya Hindi usiku wa kuamkia Jumamosi, Septemba 10, 2011

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, ameamuru maombolezo ya kitaifa kwa muda wa siku tatu kuanzia leo tarehe 11 Septemba, 2011 ambapo bendera nchini zitapepea nusu mlingoti.
Aidha, kufuatia msiba huo, Mheshimiwa Rais, ameahirisha ziara rasmi ya kiserikali ya siku tatu nchini Canada ambako alikuwa amealikwa na Gavana Mkuu wa nchi hiyo, Mheshimiwa David Johnston.
Katika ziara hiyo iliyokuwa ifanyike kuanzia tarehe 14 – 16 Septemba, 2011, Mheshimiwa Rais angekutana pia na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Mheshimiwa Stephen Harper. Mheshimiwa Rais ameiomba Serikali ya Canada kupanga ziara hiyo kwa tarehe za baadaye.
Rais alitembelea majeruhi katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, Zanzibar, kuwajulia hali, baada ya ajali hiyo. Akiwa katika ziara hiyo ya majonzi aliarifiwa kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano ilikuwa imechukua maamuzi kadhaa kukabiliana na hali ya ukoaji wa watu katika ajali hiyo.
Miongoni mwa hatua hizo ni pamoja na kuchangia kiasi cha sh. milioni 300 ili kusaidia zoezi hilo ikiwa ni pamoja na kusaidia kusafirisha na kuzika miili ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo. SMZ imetoa sh milioni 100 kwa shughuli hiyo.
Serikali ya Muungano pia imeamua kukubali msaada wa wapigaji mbizi kutoka Afrika Kusini kwa ajili ya kusaidia kufanya tathmini ya jinsi meli ilivyozama na kuokoa maisha ya watu ambao watakuwa wamebanwa ndani ya meli hiyo.
Aidha leo, Septemba 11, 2011, Kamati ya Taifa ya Ulinzi na Usalama itafanya kikao chake mjini Zanzibar kuzungumzia hali ya ajali hiyo kwa maana ya kupata maelezo kamili kuhusu ajali hiyo, kupokea ripoti ya ajali, kufanya tathmini ya ripoti hiyo na kutoa maelekezo ya jinsi ya kukabiliana na hali ya sasa na hali ya baadaye ya usafiri wa maji nchini.
Hata hivyo kabla ya kikao hicho, tayari Rais Kikwete ameamua kufanyika kwa uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha ajili hiyo.

Kwa habari zaidi na Picha
BOFYA HAPA

MAMIA ya wananchi wakiwemo viongozi wakuu walimiminika katika viwanja vya Maisara na Hospital ya Mnazi mmoja pamoja na bandari kuu ya zanzibar ili kwenda kuona na watambuwa watoto wao wazee wao ambao walikuwepo katika meli iliyopata ajali huko Nungwi ikielekea kisiwani Pemba hapo jana

Waliomiminika katika sehemu hizo kutoka sehemu mbali mbali za Unguja kunafuatia habari zilizoanza kutangazwa jana katika vyombo mbali mbali vya habari kwamba chombo cha Spice kimezama na ni kwamba kilikuwa kimechukuwa abiria kikielekea Pemba

Kwa mujibu wa habari zilizokuwa zikisimuliwa na baadhi ya wananchi waliofika hapo maisara wamesema kuwa suala kubwa lililochangia kutokea ajali hiyo ni kuwa vyombo vimechoka sana na wengine wamesema kuwa kujaa sana kwa chombo hicho hapo jana pia ni sababu ambazo zilichangia tukio hilo

Katika Viwaja vya Maisara umati wa watu ulikuwa umejaa kupita kiasi halikadhalika hata Hospital ya Mnazi mmoja umati ulikuwa umejaa vikle vile lengo kubwa la kuwepo hapo ni kuona na kuwatambua vijana wao ambao wameruhiwa na ambao wanapata matibabu

Halikadhalika umati mkubwa ulikuwa umejazana sana katika bandari mkuu ya Zanzibar ambapo maiti na majeruhi wa ajali hiyo walikuwa wakifikia hapo kutoka sehemu ya tokeo

Kufuatia ajali hii hii itakuwa mara ya tatu
katika pindi cha nyuma meli ya MV Fathi ilizama 29/5/2009 ambapo watu kadhaa wafariki dunia na baadhi ya mizigo ilpotea kutokana na ajali hiyo iliyotokea hapo nyuma, pia maafa makubwa ya MV Bukoba 21/5/1999

Kufuatia tokeo hilo wananchi wa zanzibar leo walikuwa wamejikusanya vikundi kila sehemu kuzungumzia tukio hili ambalo limetoke hapo jana likiwa limeacha majonzi makubwa kutokana na msiba huo uliotokea hapa zanzibar




iotokea hapa
source; http://www.latestnewstz.blogspot.com/

Saturday, September 10, 2011

SIMANZI KUBWA KWA TAIFA, Meli ya Abiria zaidi ya 600 imezama baharini usiku wa kuamkia leo zanzibar....!

Meli ya Spice Islander iliyokuwa ikifanya safari zake toka Unguja kuelekea Pemba ikiwa imezama ktk bahari ya Hindi, Malindi usiku wa kuamkia leo ambapo mpaka sasa inasadikika watu waliojeruhiwa wako zaidi ya 267 katika Hospital ya Mnazi mmoja Zanzibar, na maiti zaidi ya 113 zimeshapakikana na kuhifadhiwa ktk uwanja wa Maisara huku ndugu na jamaa wakizitambua


Sehemu ya umati wa watu wakiangalia kwa majonzi uokoaji ukiendelea ktk pwani hio



Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein katikati akiwa na Makamu wa Kwanza wa Rais na Mama Mwanamwema Shein kushoto wakionekana wenye majonzi kabisa wakati walipokwenda kushuhudia majeruhi wa ajali hiyo pamoja na maiti


Vikundi vya waokoaji bado vinaendelea na kazi hio viongozwa na wanajeshi wa KMKM, JKU na wengine wakiwamo wavuvi wa maeneo ya karibu

MUNGU AZILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO ZA WOTE WALIOFARIKI KTK AJALI HIO, NA KUWAPA NAFUU MAJERUHI WA AJALI HIO

Friday, September 9, 2011

NAS Bizness; Msanii na Mtayarishaji wa mziki anayekuja kwa kasi

Jina kamili jamaa anafahamika kama Jonas Steven aka NAS Bizness, ni producer wa muziki ktk Studio za Pamoja Records zilizopo Kinondoni jijini Dar es Salaam. Mchizi alianza kutengeneza beats na kufanya mautundu ktk mixing kitambo kidogo akipitia ktk Studio mbambali za hapa Bongo kabla ya kupata dili ya kurekodi na kufanya mixing ktk kanisa moja pande za Nairobi Kenya

Moja ya Kazi nzuri alizozifanya ni pamoja na ngoma mpya ya kina Dullayo, Joslin, Mon G na XDizo (Makavulive) inayoitwa "Mambo mambo" ambayo tayari imeshaanza kuchezwa ktk vituo mbalimbali vya redio. Pia NAS-B amefanya kazi kibao zilizopo ktk Album mpya ya 20 PERCENT km "Zali zalina" na nyingine kibao, "Narudi kijijini" ya BEST NASA, "Binadamu" ya Peace Maker na ngoma za NEY wa Mitego.

Utapata kuskia pia ngoma mpya kutoka kwa Dullayo inayoitwa "Nimeamua" ambayo Nas B yuko mbioni kuimalizia Mixing ikiwa ktk beat kali la mtindo wa ki-south.




Kwa Upande wa pili Nas B ni msanii wa Bongofleva na tayari ameshaachia tracks kadhaa ktk vituo mbalimbali vya redio. Kuna nyimbo amefanya na 2O Percent inayoitwa "Ngombe wa Maskin Azai", 'Dua la Kuku" na nyinginezo

Weekend hii NAS B anatarajia kuanza kwa utengenezaji wa Video ya nyimbo yake mpya 'Dua la kuku" ambapo atashoot video hio ktk viunga vya Sinza pande za Palestina.

Wasanii wakongwe wa dansi kuimba BongoFleva mkesha wa Miaka 50 ya Uhuru..!

Wasanii wa Bongofleva na wanamuziki wakongwe ktk mkutano na wanahabari wakielezea onyesho lao la pamoja kusherehekea miaka 50 ya Uhuru.

Wanamuziki wa zamani na wa kizazi kipya, wanatarajia kuungana kuimba jukwaa moja Desemba 8, mwaka huu katika mkesha wa miaka 50 ya Uhuru. Katika onesho
hilo,
wanamuziki wa zamani wataimba nyimbo za wasanii wa kizazi kipya na pia wasanii wa sasa nao wataimba nyimbo za zamani.

Mwenyekiti wa Sauti za Kale Waziri Ally, alisema wanatarajia siku hiyo kutakuwa na burudani ya kukata na shoka kwa kuwa kutakuwa na muziki wa zamani na wa kisasa.

“Hakika itakuwa burudani ya aina yake kwa mashabiki na Watanzania kwa ujumla, kwani muziki utakaotoka hapo utakuwa na ladha ya ina yake,” alisema Mwenyekiti huyo.

Alisema katika onesho hilo, wao wakongwe wamepania kuwaonesha wanamuziki wa sasa, kwamba wao wanaujua ujana na uzee pia huku wanamuziki wa sasa wakiwa wanajua ujana na si uzee.

“Sisi wote tuna lengo moja la kuungana na kupanga nini tunataka kufanya katika onesho hili la miaka 50 ya Uhuru, litakalorindima Diamond Jubilee,” alisema.

Naye mwanamuziki nguli nchini King Kikii, alisema siku hiyo patakuwa hapatoshi katika burudani hiyo, kwani wanajiandaa kuhakikisha wanakumbushia enzi za zamani ambapo mazoezi yataanza wiki ijayo.

Damon Dash ana msala mwingine wa kuuza pombe bila Kibali....!


Mnyamwezi Damon Dash (40) Mjasiriamali na mwanzilishi wa Roc-A-Fella Records, ye na washirika wake wana msala wakituhumiwa kuwa "kero kwa umma" pia wana mashtaka sita ya kuhifadhi na kuuza pombe bila leseni.

Japo kuwa aliyahama makazi yake DD172 huko Tribeca New York mwezi Juni, Damon Dash kisheria bado yupo kwenye msala. Mara ya kwanza walikamatwa DD172 baada ya kukiuka kanuni za pombe mwezi Novemba 2010 na Mei.

Ukiukwaji ulifanyika kwa namna ya wazi na sifa mbaya huku majamaa wanaonekana kuendelee na 'biashara kama kawaida' katika majengo hayo.