Monday, January 16, 2012

R . I. P Mo CHELLAH

SONG: For My Brother (R.I.P. MO CHELLAH)
Written By Ezden The Rocker


VERSE I:

Kilio huanza mfiwa, ndipo wa mbali wanaingia/
Hizi siku zinahesabiwa, huwezi jua tapotimia/
Umeniacha na maneno, kama baridi na urusi/
kinywa jumba la maneno, kamwe nisiongee tusi/
Beef zilotokea, vijambo kwenye mitaa/
Mwanga nakuombea, haya maisha ni vita/
Ulinipa nyingi sana, changamoto kwa Freestyle/
Leo tumetengana, battle zangu haziwezi fika/
Wahenga walishasema, Chanda chema huvikwa pete/
Ma-Mc walikusoma, kwa mistari isio na ubwete/
Kitanda usicholala, huwezi jua kunguni wake/
Machungu ni zaidi ya msala, subiri matokeo yake/
Tulisaka sana heshima, Na hela sio publicity/
Mashairi yenye vina, walipiga salute - Ti!/
Mashavu tulikomba, kwa mashairi tuliwabonda/
Ndugu sa msijekonda, cha msingi tuzidi kuomba/


VERSE II:

This is for my brother, from another mother/
Nauchungu siisomi ladha, lakini nakaza stanza/
Kumbuka mara ya kwanza, mimi nafika mwanza/
Wewe kina P.M.P na Flexx wa Mwanza Kwanza/
Mlinipokea vizuri, A2P Mitaa ya Uhuru/
Vitu vingi tuliendana, hasa hii mitindo huru/
Sina cha kufanya, Mungu tu namshukuru/
Mi na Hip Hop tashikana, kusongesha hili duru/
Kivuli cha fimbo, hakimfichi mtu jua/
Leo naimba wimbo, kesho sijui ntakapokua/
Tuangalie matendo, huenda ndo yatatuokoa/
Umenipiga nembo, moyoni sitoiondoa/
Alichoandika Mungu, lazima kitimilike/
Yes moyoni nina uchungu, Mo Chella peponi ufike/
Utabaki kumbukumbu, Milele usisahaulike/
Documentary ya MLAB ile alotu-shoot Duke/

No comments:

Post a Comment