World News

Friday, March 2, 2012

ChriSs brOwn amwAndalia mpenzi wake chAkula cha UsikUHii si kawaida kibongo bongo kwa mwanaume kuingia jikoni na kupika,kwani ukionekana tayari utapatiwa jina la Mume bwege.Lakini hii ni kawaida sana kwa nchi zilizoendelea japo kwa wasanii wenye majina si kawaida kutokana na kubanwa na kazi nyiingi za kijiendeleza...Wiki iliyopita Magazeti mengi yaliandika kwamba Chriss brown anaelekea kumrudia mpenzi wake wa zamani Rihana baada ya kutoa singo mbili,''birthday cake''ambao upo katika album ya Rihana na ''Turn up the music'',ambao uko katika album ya Chriss brown,wawili hawa walishirikiana pamoja kutengeneza remix za nyimbo hizo.Mpenzi wa Chriss Brown Karrueche Tran hakushtushwa na hilo kwani alisema uhusiano wao si wa kujificha na kila mtu anatambua,aliongezea kwa kusema ile ni kazi tuu wala hakuna chochote kinachoendelea kati mpenzi wake na Rihana  na wanapendana.Kuthibitisha hili Chriss Brown alionekana jana usiku akimwandalia msosi wa maana mpenzi wake  huyo kama picha zinavyoeleza...kwa hiyo mnaosema Chriss anarudi kwa Rihana hilo msahau

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...