World News

Friday, March 23, 2012

D'banj mambo yake yanazidi kuwa msuano!!

D'banj and Big Sean
 
 Hivi karibuni ali-saini na studio ya Kanye West, Good Music. Akatoa remake ya wimbo wake, ‘Mr. Endowed' kwa kushirikiana na Snoop Dog ambayo ilikuwa ni bonge moja ya ngoma.

Ingawa studio yake binafsi, Mo Hits, inaonekana kufa baada ya kutengana na mchizi wake Don Jazzy, pamoja na wasanii ambao walikuwa kuwakilishwa na hiyo studio kuonekana kuwa katika utata, yeye anazidi kupanda chati na kuwa matawi ya juu zaidi.

Video yake rasmi ya goma kali la  'Twist Oliver' wimbo tayari imekuwa maarufu sana, imewashirikisha wakali Big Sean, Pusha T, na Kanye West, na pia imepiga hatua kubwa kiasi cha watu wengi kuizungumzia.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...