World News

Tuesday, April 17, 2012

Double J ya Jimmy Master Kuingia Sokoni


MSANII kwenye tasnia ya filamu nchini Jimmy Mponda 'Jimmy Master'amesema yuko mbioni kuingiza sokoni ujio wa filamu yake mpya iitwayo 'Doble J'.

Mbali na ujio huo wa sasa , 'Jimmy Master'ambae  alishawai kutikisa na filamu ya 'Misuko Suko' ambayo ilitoka kuanzia Party 0ne hadi Party three.

Akizunguza jijini Dar es Salaam'Jimmy Master' alisema kuwa ujio huu wa hivi sasa wa filamu hiyo huko chini ya Kampuni yake iitwayo Jimpo Wood Company LTD .

"Huu ni ujio wangu mpya kwa sasa baada ya kujipatia mashabiki kwenye filamu za 'Misuko Suko' Party one hadi three,"alisema 'Jimmy Master'.

Awali 'Jimmy Master' alianza kujipatia mashabiki wa filamu kupitia filamu kama 'WOSIA' ambayo pia alifanikiwa kuibua vipaji vya wasanii wa Bongofleva.

Ambapo wasanii kama Abubakari Katwira Q- Chilla pamoja na Daz Edd Waliibuliwa

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...