World News

Tuesday, April 17, 2012

ISHA Mashauzi..... Awashukuru Wadau, Mama yake mzazi, Thabit Abdul
Isha Ramadhani, muimbaji wa bendi ya Taarab Mashauzi Classic na Mshindi wa Tuzo ya Wimbo Bora wa Taarab Tanzania 2011/12 akiongea na Blogu ya Dida huku akifanya shopping Dida Classic Boutique 'Mamaa wa Mashauzi' ametoa SHUKURANI za pekee kwa Wadau wote wa muziki waliompigia kura na wote waliokosa hio nafasi kwa kuibuka mshindi, bila nyinyi asingeweza kufika hapo alipofika.

Pia amemwagia sifa na kumpongeza sana Thabiti Abdul kwa utunzi bora wa nyimbo ya NANI KAMA MAMA kiasi cha kutwaa Tuzo kupitia yeye


Wengine aliowashukuru ni Mama Yake Mzazi 'Rukia Juma' ambaye ndiye aliyeimba nae ktk wimbo huo uliowapatia sifa kubwa sana na kupendwa na mashabiki wa Taarab hadi kupewa Tuzo hiyo, bila kuwasahau wasanii wote wa Bendi yake ya Mashauzi Classic kwa ushirikiano mkubwa walionao ktk kuliendeleza gurudumu hili hasa ukizingatia bendi bado ni changa
.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...