World News

Monday, April 16, 2012

MISS UTALII KINONDONI 2012 KUFANYIKA CLUB SUNCIROMiss Utalii 2011, akipokea zawadi kutoka kwa mbunge wa Kinondoni mh. Idd Azzan
Miss Utalii Kinondoni na Miss Utalii Tanzania no. 5 ktk picha ya pamoja na Mh. Anna Makinda, Samwel Sitta, Mkurugenzi wa Konyagi Mr. Mgwaza,

Shindano la kumpata Binti wa Utalii Kinondoni 2011/2012(Miss Utalii Kinondoni 2011/2012 ngazi ya wilaya limepangwa kufanyika katika ukumbi wa kisasa na Club ya kimataifa ya Sinsiro,iliyoko Shekilango Sinza.Shindano hilo limepangwa kufanyika siku ya Ijumaa tarehe 25 Mei 2012 na kushirikisha mabinti 25 kutoka katika majimbo yote ya wilaya ya Kinondoni.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na mkurugenzi wa Miss Tourism Tanzania Organisation wilaya ya Kinondoni Pius Yalula,ambao ndio waratibu na waandaaji wa shindano hilo, washiriki wote wanatarajia kuanza kambi ya mazoezi katika ukumbi huo siku ya Jumatatu Mei 1,2012. Miss Utalii Kinondoni 2010/2011 Sophia Dioa ambaye pia ni Miss Utalii Dar es Salaam 2010/2011 na Miss Utalii Tanzania 2010/2011.Piusi Yalula alibainisha kuwa ni mpango mkakati wa Miss Tourism Tanzania organisation mwaka huu, wa kuwafuata watanzania hususani vijana katika maeneo yao ya burudani,ili kuwahamasisha juu ya utalii wa ndani. Ndio maana fainali za mwaka za Miss Utalii Kinondoni ,tumeamua kuzifanyia katika Club ya Sunciro, ambako tunaamini kuwa vijana na watu wa rika mbalimbali wanapenda kwenda katika kumbi na club za aina hiyo kwa ajili ya burudani na mapumziko ya wikendi. Utafitin uliofanywa na kitengo chetu cha masoko umebaini kuwa ili dhana ya utalii wa ndani iweze kufanikiwa ni lazima tuanze na watu hususani vijana ambao tayali ni wapenzi wa burudani na wako tayali kutumia sehemu ya pato lao kwaajili ya burudani na mapumziko ya mwishoni mwa wiki. Tutatumia shindano hili la Miss Utalii Kinondoni 2010/2012 kuwahamasisha wapenzi wa burudani, vijana  na watu wa rika zote kujenga tabia ya kwenda kuembelea vivutio vya utalii nchini ,hususani vya wilaya ya kinondoni na pia kuwaelimisha wao na jamii kuwa Utalii na Burudani kama zilivyo burudani nyingine na ni fulsa nzuri ya mapumziko ya mwishoni mwa wiki, tena wakati mwingine kwa garama ndogo,kwani Serikali na mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) wameweka bei isiyo zidi shilingi 1500 kwa mtu mzima na shilingi 500 kwa watoto.

Fomu kwaajili ya kushiriki shindano hilo zinapatikana katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam ikiwemo Sunsiro Club Shekilango, Zizzu Fashion Victori,Sea Boys Magomeni,BM Saloon Kinondoni, Dar es Salaam City Collage Kimara,Chicken Hut mlimani City, Angel Saoon Sinza,Coco Beach OyterBay  na katika ofisi za Miss Tourism Tanzania Organisation zilozoko Ilala Bungini na Kimara Dar es Salaam.
Pous aliongeza kuwa fainali za mwaka huu za Binti/Miss Utalii kinondoni 2011/12 zitakuwa ni za kipekee kutikana na kamati ya maandalizi kujipanga vilivyo ,ili kuhakikisha huwa taji la Miss/Binti Utalii Dar es Salaam linabaki kinondoni na pia kuhakikisha tunachukua taji la taifa la Miss /Binti Utalii Tanzania 2011/12 mwaka huu. Sifa za kushiriki shindano la Miss /Binti utalii Tanzania ni pamoja na Elimu isiyo pungua kidato cha sita au yenye kulingana nayo, uwezo wa kuzungumza kiswahili fasaha,urefu wa angalau setimita 160 au zaidi, raia wa tanzania, ngozi na rangi asili,jinsia halosi ya kike, umri usio pungua miaka 18 wala kuzidi miaka 27 na awe ni mwenye tabia na mwenendo ,tabia njeama na mfano wa kuigwa katika jamii.
Asante,
Pius Yalula
Mkurugenzi Miss Utalii Kinondoni
Miss Tourism Tanzania  Symbol Of National Heritage - Do Value Added Pageant
"Lets Visit & Promote Tanzania National Parks -Tourism is Life ,Culture is Lining"
Regard,
Gideon E.G. Chipungahelo
PRESIDENT / C.E.O
Hotline: + 255 - 715/754/773 - 318 278.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...