World News

Wednesday, May 2, 2012

Bondia Fike aachana na masubwi kwa mapenzi ya mkewe!!

BONDIA na mtunisha misuli maarufu Fike Wilson mwishoni mwa wiki iliyopita amefunguka na kudai mke wake anamchanganya katika mapenzi ndio maana alisikiliza maneno ya mama mkwe na kuamua kuweka kando kazi yake.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam Wilson alisema kuwa aliacha  mchezo huo aliodai ni wa kifo  mara baada ya kuumia katika mpambano wa mwishoni kabla ya kustaafu masuala hayo baada ya kuwa ameumia bila kupigwa konde lolote ulingoni.

"Kabla ya kuamua mie mwenyewe kuacha kupanda ulingoni , mama mkwe wangu ndio aliye sema niache ndondi kwani siku hiyo ya mpambano wangu mwaka 2005 nilijikwaruza wakati wa mchezo wangu huo nikaumia ulingoni jeraha lilikuwa kubwa lilimsikitisha mama mkwe,"alisema Fike.


Fike anasema sababu ya jeraha hilo ambalo si lakupigwa konde badi lilitokana na kujikwaruza kwenye kamba za kuegamia katika masumbi ulingoni,tangu hali hiyo ilipotokea ndipo mama mkwe wake akamshauri aache ndondi.

Nyota yake haikuanzia moja kwa moja katika ngumi kama wanamichezo wengi wanavyomfahamu leo, bali katika mchezo wa kutunisha misuli uliomwezesha kutwaa taji la Mr Tanzania.

Lakini baadaye alipojitosa rasmi kwenye ngumi za kulipwa alidhihirisha hakuna mtu wa kumzuia.
Wilson mzaliwa wa Mbeya yeye ni mwenye diploma katika masuala ya Fitness na Nutrition aliyoipata Marekani.

Kwa wale ambao si wapenzi wa ngumi basi jamaa alisha fanya movie iitwayo ' Power of God', iliyowashirikisha wasanii nyota kibao ndani ya movie hiyo na baadaye akatoka na filamu nyingine iliyoitwa
'Lost Dream' na kufanya kweli anga za movie.

Aidha jamaa huyo mwenye mwili wa mazoezi alisema katika familia yake kwa sasa wote ndani ya nyumba yao ni wasanii kwani ameshilikisha mke pamoja na watoto katika kuuvaa huusika ndani ya movie zake zote mbili.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...