Thursday, June 14, 2012

Baada ya Diamond na Dj Fetty kupagawisha BBA StarGame, AY kudondoka tena ktk Show ya Jumapili hii!

 
Msanii wa muziki wa Hip Hop (Bongo Flava) nchini ambaye anafanya vizuri ndani na nje ya Tanzania, Ambwene Yessayah (AY), anakuwa msanii wa pili kuiwakilisha vyema na kupeperusha bendara ya Tanzania wikiendi hii pale Johannesburg katika  show ambayo anatarajia kuifanya siku ya jumapili hii tarehe 17/06/2012 kwenye Big Brother Star Game.

AY anatarajia kuondoka nchini kuelekea Afrika Kusini siku ya jumamosi na akiongozana na Mwana Fa na Arthur pia ataungana na Sauti Sol kutoka nchini Kenya kwa pamoja siku hiyo watapiga show hiyo.Hii itakuwa kwa mara ya 2 AY kufanya show katika Big Brother awali ilikuwa 2008.

AY pia yupo mbioni kuachia wimbo mpya wa “Party Zone” akiwa ameshirikisha Marco Chali kutoka Mj Records. Wimbo huo ambayo umekalimika hadi ukuchukuaji wa picha( Video). Ambapo video imetengenezwa na kampuni ya The God Father Production ambao wapo Afrika kusini, ni kampuni ambayo imefanya kazi na wasanii wengi sana wakiwemo P Square,J Martin, Mr. Flavor,Akon,na wengine wengi, Na gharama ya video hiyo imegharimu  dolla za kimarekani elfu ishirini (20,000), sawa na milioni thelathini na mbili za kitanzania (32,000,000). Na wimbo huo wa Party Zone anarajia kuwachia mapema week ijayo.

Aytanzania.com
 

No comments:

Post a Comment