World News

Thursday, June 14, 2012

DULLAYO AWATAJA WASANII WATATU WANAOIWAKILISHA "MAKAVULIVE"

Dullayo ambaye ni kiongozi wa Clik ya Makavulive, amewataja wasanii watatu wanaoiwakilisha Familia ya Makavulive ktk Muziki ambao ni yeye mwenyewe DULLAYO, MON-G na EASY MAN.

 Ktk Interview aliyofanya live na Presenter wa Uhuru Fm 'Soggy' wakati anaitambulisha nyimbo mpya ya Makavulive inayoitwa "FUNGUA" waliyomshirikisha Joslin, Dullayo aliulizwa na Soggy kuwa Makavulive ni nini, akasema "Makavulive ni Chama kubwa kama familia ambamo kuwa watu wengi sana ambao wanahusiana nalo na kila mmoja ana shughuli tofauti na muziki kwa ajili na maisha ya kila siku"

Mon-G & Dullayo
"Ila kwa upande wa muziki kwa sasa tupo wasanii watatu tunaowakilisha Makavulive ambao ni Dullayo, Mon-G na Eazy Man ambaye yeye ame-base sana ktk style ya Mnanda au mchiriku lkn pia yupo Makavulive"

Eazy Man

Pia Dullayo amesema kwa sasa wapo serious kukamilisha Project yao ya Kwanza kama kundi na tayari wameachia ngoma kali mpya kutoka kwa P FUNK "MAJANI" wa BONGO RECORDZ na upigaji wa picha (Video) ya nyimbo hiyo utaanza muda sio mrefu.

Album ya kwanza ya Dullayo - 2008

 Huku kila mmoja akiendelea na mitikasi ya Album yake ambapo yeye mwenyewe anakamilisha album yake ya pili baada ya IMANI aliyotoa 2008, pia Eazy ameshamaliza ya kwake na Mon-G naye yuko mbioni kukamilisha ya kwake.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...