Na Mwandishi Wetu
MSANII wa muziki wa kizazi
kipya nchini Nasib Adbdul ‘Diamond’ anatarajiwa kupamba shindano la kumsaka
Miss dar Intercollege 2012 linalotarajiwa kufanyika Juni 22 kwenye ukumbi wa
Makumbusho ya Taifa , uliopo mkabala na chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
Mratibu wa shindano hilo Dina Ismail alisema jana kwamba mbali na Diamond,
onyesho hilo 
pia litapambwa na burudani kutoka bendi ya Skylight iliyopo chini ya mshiriki
wa Tusker Project Fame mwaka juzi, Anneth Kushaba.
Alisema
 maandalizi ya
shindano hilo 
yanakwenda vema ambapo warembo 14 watakaosghiriki  wanaendelea na 
mazoezi katika hoteli ya  The Grand Villa iliyopo Kijitonyama jijini Dar
es Salaam
 “Mwaka huu tumejipanga vema kuhakikisha mmoja
ya warembo kutoka Miss Dar Intercollege 
anafanya vema katika fainali za Miss Tanzania ,”alisema Dina.
Warembo watakaoshiriki
shindano hilo  wanatoka vyuo vya  Biashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ) na
Time,  Ustawi wa Jamii,  Usimamizi wa Fedha (IFM)  na Chuo Kikuu huria (OUT ambapo taji
linashikiliwa na Rose Msuya kutoka IFM, huku mshindi wa pili wa mwaka jana,
Blessing Ngowi alitinga fainali za Miss Tanzania.
Dina aliwataja warembo hao
kuwa ni pamoja na Veronica Ngota, Rose Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda  Edward, Diana Nyakisinda, Neema Michael,
Veronica Yollla, Jacquiline Cliff, Sharifa Ibrahim, Natasha Deo, Saada
Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan.
Shindano hilo limedhaminiwa
na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Redd’s,Dodoma Wine, Ndege
Insurance, Skylight Band,Lamada Hotel, Screen Masters,Makumbusho ya Taifa,
Mustafa Hassanali, Shear Illusions, Lamada Hotel,Grand Villa Hotel, Sporti
Kizaa zaa, Clouds Fm na blog za Michuzi, Mamapipiro, Bin Zubeiry,Mtaa kwa Mtaa
na Fullshangwe.

No comments:
Post a Comment