World News

Friday, June 15, 2012

TISHO BOY Engineer, Msanii anayekuja kuiteka Afrika Mashariki

Tisho Boy (Muhindi Kutisha) ni msanii chipukizi wa kizazi kipya  mwenye uwezo wa kuimba na kufoka(Rap) ambaye pia ni Mwanafunzi wa Computer Engineering Nairobi Kenya
Alianza sanaa ya uimbaji akiwa chekechea wakati huo akishiriki katika kwaya ya shule. Swala la uimbaji halikuwa limechipuka sana kwani maigizo yalimchukuwa muda sana. Alipenda ushairi na fasihi kwa ujumla na haswa mwanzo wake, tungo za kishairi akazifanya nyimbo. 
Wimbo wake wa kwanza Mpenzi Nakupenda aliomshirikisha 2M, haukumfurahisha lakini ikawa changamoto chanya kwake kama kawaida ya wasanii chipukizi wanapochupuka.
 Alifwata na Nipe Flow ambao amemshirikisha Farisayo(Emmanuel Karisa) pamoja na Lidwati na Tuna akimshirikisha Farisayo vile vile ambazo amezifanyia UGC (Orynx Music) Production, Kenya kwa mitindo ya Kapuka/Genge. Anatazamia kufanya video hivi karibuni.


Tisho Boy ni Mwandishi pia wa Riwaya na Tamthilia. Riwaya yake 'Kumbukumbu za Kutisha' anaitazamia kuipiga chapa na matbaa mojawapo nchini Kenya. Pia yeye hutunga na kughani mashairi na vilevile anakusudia kutoa Diwani yake ya Mashairi 'Kabwela la Bara' mwakani.

Alizaliwa 1990, Desemba 23 nchini Kenya. Asili yake ni ya Kitaita na Kihaya.(Bongo)

Anapenda muziki, kucheza na kutazama soka, shabiki mkubwa wa Chealsea, kutazama Bongo Movie na ana ndoto ya kufanya Bongo Movie siku za halafu. Ana uraibu na maswala ya tarkalishi sana na kuimba. 

Farisayo

Tuna_Tisho Boy ft Farisayo.
Tuna ni wimbo ulioimbwa kwa mtindo wa ragga/Dancehall/Kapuka. Ni Klub song ambayo inazungumzia kula bata haswa walengwa wakiwa vijana na yeyote mwenye uwezo wa kujirusha. Ina maudhui ya starehe ya klub na pia inakashifu wenye jicho na chuki. Kwani wapende wasipende, tunajirusha. Imefanywa UGC Production na Producer Miwo nikimshirikisha Farisayo( Emmanuel Karisa)
http://www.reverbnation.com/open_graph/song/13545738, Unaweza kuskiza na Ku-download free nyimbo hii ktk Playlist ya Makavulive hapo juu.


Nipe Flow
Nipe flow ni track ambayo ina maudhui ya mapenzi. Kuna binti nampenda lakini kuna wenye kijicho wenye wivu. Nawakausha kwa track hii kwa kumwambia binti huyu anipe flow nizidi kuringa(Kujiroll)

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...