World News

Wednesday, June 20, 2012

Warembo Miss Dar Intercollege kusugua kisigino na Twana leo!!


Na Mwandishi Wetu

WAREMBO wanaotarajiwa kushiriki shindano la Miss dar Intercollege 2012 jumatano wanatarajiwa kujivinjari katika ukumbi wa kimataifa wa Club Bilicanas iliopo katikati ya jiji la Dar es Salaam.

Shindano hilo limepangwa kufanyika Ijumaa ya Juni 22 katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa uliopo mkabala na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ambapo msanii wa bongo Fleva Nasib Abdul ‘Diamond’ anatarajiwa kutumbuiza.

Mratibu wa shindano hilo Dina Ismail amesema leo kwamba, warembo hao watapata kuhudhuria onyesho maalum la bendi ya African Stars "twanga Pepeta' kupitia usiku wa Mwafrika unaorindima kila jumatano katika klabu hiyo.

Dina alisema uongozi wa Bilicanas Group umewaalika warembo hao ili kuweza kuburudika pamoja na mashabiki wa muziki wa dansi nchini kwa lengo la kujipoza baada ya mazoezi yao.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...