Friday, September 7, 2012

BINTI ANATAFUTA UMAARUFU BONGO KUPITIA MIGONGO YA WATU NA UDAKUZI

kutoka gazeti la Udaku 

Dogo anayedaiwa kuvunja ndoa ya watu ni kama anatafuta Ustaa tu au umaarufu kupitia magazeti ya udaku, ukweli ni kwamba binti huyu anayefahamika kwa jina la Peris ( kumbe anaitwa Tecla Benedict) hajavunja ndoa ya G na hana uhusiano nae kutokana na habari zilizopatikana kwa muhusika

Awali kabla hajajiunga na chuo cha Magogoni, Peri msanii chipukizi alikutana na G baada ya kuletwa na msanii mwenzie wa kiume MON G ambaye husaidiwa kazi zake na bwana G, akimpamba kwamba anajua kuimba huku lengo likiwa kuingiza sauti ktk wimbo wao mpya  unaoitwa Fungua, G akampa go-ahead Mon binti akapelekwa studio lakini alishindwa kuimba vile prodyuza alivyotaka, baadae Mon akamuombea nafasi nyingine Peri labda itakuwa nafasi yake ya kutoka sasa ombi lilikubaliwa na kuambiwa asubiri kidogo, baada ya yeye mwenyewe kusumbua sana kwa simu akapatiwa nafasi ktk studio nyingine ambapo aliimba wimbo wake akisaidiwa na Mon G wimbo ulishakamilika lkn bado haupo ktk viwango vya kupigwa redioni (kwa mujibu wa wataalam wa muziki) hivyo binti ikabidi aachwe, G na vijana wake wakaendelea na project yao ya Makavulive.

Zikikanushwa Habari iliyoandikwa na Udaku, Amani Alhamisi 6 sept. 

1. Kuhusu sms kudakwa na mke, ni kweli yule binti alikuwa akiandika sms kuulizia ahadi aliyopewa kupelekwa studio baada ya ile ya kwanza kuchemka, alipopigiwa simu alijitetea kuwa anaulizia tu kazi kusaidiwa kuingia studio baada ya kuona kimya kingi ila kutokana na kwamba alikuwa akiandika kimitego ya mapenzi ndio mana alipigwa biti kali na mke

2. Kwamba alikubali kuwa ana uhusiano na G, na kwamba G hajawahi kumuona na Pete hivyo hakujua kama ni mume wa mtu... huo ni uzushi dhahiri sababu huyo binti kabla ya kukutana na G watu waliomuunganishia nafasi hio walimwambia kuna bosi wetu anaetusapoti ambae ni G mume wa mtangazaji, G mara nyingi watu tunapokutanaga akiwepo na huyo binti 'sijawahi kumwona G bila pete yake ya ndoa amethibitisha Mon G ambaye mara zote huwa ndio kiunganishi cha watu kukutana na ndio anayehakikishaga huyo binti kafika na kumrudisha kwao Mbagala hivyo kabla hajamuona G alijua kabisa G ni nan, mbali na kazi zake G hupenda kuandaa shows na kusapoti sanaa za muziki hasa wasanii wa Makavulive 


G ameshangazwa sana na habari hizo kwanin watu wa udaku wanajiandikia tu ishu nyeti kama hizo bila kujali impact yake ktk jamii. Anaamini kuwa labda kuna mtu/watu nyuma ya huyo mtoto anayesababisha huu upuuzi!

 Pia kachukua nafasi hii kuwaomba radhi ndugu, jamaa na marafiki kuwa wastahimilivu kutokana na huo udaku kuwa hawapaswi kuamini habari km hizo unless otherwise muhusika ameongea mbele yao....

No comments:

Post a Comment