Thursday, January 17, 2013

VING'AMUZI VYAKWAMISHA WASANII KUSAMBAZA VIDEO ZAO MAPEMA



Mkali wa ‘Usinicheke’ Keisha amesema ameshindwa kuachia video yake mpya kutokana na mfumo wa matangazo ya televisheni wa digitali kuwaacha nje mashabiki wengi wa muziki hasa katika jiji la Dar es Salaam.


Keisha ni miongoni mwa wasanii wengi walioingiwa na moyo mzito wa kuachia video zao kipindi hiki kwa hofu kuwa itatazamwa na watu wachache kwakuwa watu wengi bado hawana ving’amuzi.

Akiongea na E-news ya EATV, Keisha amesema hali hiyo haijamuathiri yeye tu bali wasanii kibao akiwemo Hemedy Phd ambaye naye anasita kuitoa video yake

Amesema kulingana na mambo yanavyoenda, anaweza kuiachia hivyo hivyo, ila wasiwasi wake mkubwa upo kwa wale wenye uwezo wa chini ambao wanapenda kazi zake.

No comments:

Post a Comment