World News

Thursday, January 17, 2013


Hitmaker wa ‘Usinicheke’ Keisha amesema ameshindwa kuachia video yake mpya kutokana na mfumo wa matangazo ya televisheni wa digitali kuwaacha nje mashabiki wengi wa muziki hasa katika jiji la Dar es Salaam.


Keisha ni miongoni mwa wasanii wengi walioingiwa na moyo mzito wa kuachia video zao kipindi hiki kwa hofu kuwa itatazamwa na watu wachache kwakuwa watu wengi hawana ving’amuzi.

Akiongea na Enews ya EATV, Keisha amesema hali hiyo haijamuathiri yeye tu bali wasanii kibao akiwemo Hemedy Phd ambaye naye anasita kuitoa video yake.

Amesema kulingana na mambo yanavyoenda, anaweza kuiachia hivyo hivyo, ila wasiwasi wakeu mkubwa upo kwa wale wenye uwezo wa chini ambao wanapenda kazi zake.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...