World News

Wednesday, May 8, 2013

JULIO aachia Track mpya kwa ajili ya BigBrother 2013
Timewreckordz na NK production kutoka nchini Tanzania ndo maproducer wa  mwimbo wa Mshiriki waTanzania kwenye shindano la BigbrotherAfrica,show inayoonyeshwa nchi 54 barani Africa,
Mshiriki huyo Julio sasa amerudi kwenye fani aliyobobea ya Mziki na ameshafanya kazi na wasanii kibao wa bongo kama Chege chigunda,Matonya,kassim mganga,Countryboy,Chiddy benz, ukeme,Bskillz,Lamar,Lucci da don,Jokate,ROBZ..Cezeline na wasanii wa nje na pia washiriki wa Bigbrother mwaka jana...seydou soumare (Angola) Eazzy first  lady(Ghana) kwenye studio tofauti nchini na album inatoka july baada ya mafanikio ya mwimbo huu wa bigbrother


Madhumuni ya kutoa single hii ni kuwakilisha Tanzania na muziki wetu Africa na Dunia,Na pia nchi zenye kupendelea kuangalia Bigbrother ambao wafuatiliaji wa kipindi hicho cha miezi mitatu  wako zaidi ya million 20,Huu ndo muda nchi yetu itasikika kirahisi kimziki kwa nchi 54 Africa kwasababu ya nyimbo kuwa kali na vigezo vyote na kwamba inahusiana na hiyo show....Nyimbo inaitwa MR BIGBROTHER na inaoongelea bigbrother kama show,nchizi zinazoshiriki,Msiba tuliopata mwaka jana heshima kutoka kwa watanzania baada ya kumpoteza mshiriki mkubwa mwaka jana Goldie.


Huu ndio mwimbo wetu kwa mara ya kwanza katika historia ya bigbrother msanii kutoka nchini kutoa mwimbo kwa ajili ya Bigbrother Africa na support ya watanzania itatufanya kufikisha mziki wetu nje ya Tanzania na Africa. Bigbrother mwaka huu inaanza baada ya wiki mbili 26/may/2013 .Tujivunie cha kwetu na kupeperusha bendera yetu Africa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...