World News

Friday, July 26, 2013

DULLAYO kuizindua 'X100' Idd Mosi, Korogwe TANGA!

Msanii Abrahaman Kassembe "DULLAYO" atategemea kuizindua nyimbo yake mpya ya MARA MIA mara baada ya mfungo wa Ramadhani kumalizika, siku ya Sikukuu ya IDD MOSI ktk ukumbi wa Chuo cha Ualimu Korogwe TANGA. Pamoja na wimbo huo Dullayo pia atawaburudisha mashabiki na nyimbo zake nyingi zilizotamba na zinazoendelea kutamba ktk anga ya muziki ikiwemo Hawalali, Twende na mimi, Mida ya Kazi, Naumia roho na nyingine nyingi.

Tayari wimbo umeshatambulishwa na kuanza kupigwa ktk vituo mbalimbali vya redio nchini Tanzania, uzinduzi wake rasmi utafanyika siku hiyo huku akiambatana na wasanii wengine kibao wakiwemo wenzake kutoka ktk familia ya Makavulive.


Ommy G
Mon G & P the Mc
Mbali na Dullayo pia Shangwe hizo za sikukuu ya Idd Mosi zitapambwa na Ommy G, mON g, Salu B, P the Mc ambao nao watazindua nyimbo zao mpya pamoja na wasanii wengine kibao......

Baada ya Sikukuu za IDD, Dullayo amesema ataanza mchakato wa uchukuaji picha za video kwa ajili ya wimbo huo, kazi ambayo itafanywa na kampuni ya Mac Media chini ya Director Abbas Adam.

RAMADHAN KAREEM!! 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...