Yincas
mwanafunzi wa Mzumbe University ni msanii mpya anayepata insipiration
kutoka kwa Fid Q,the late Mangwea na Fabo Loso. Kwa mara kwanza namleta
kwenye ili umjua a to z kuhusu muziki wake na maisha yake kwa ujumla:
Naitwa
Mathew Yinza Telles.Nimezaliwa tarehe 08 July 1992.Jina langu la sanaa naitwa
Yincas El Legendee Nickname Killerflo.Jina la Yincas limetokana na jina langu
la Yinza ambalo idadi kadahaa ya watu wananifahamu kwa jina hilo.Ukiachana na
mzik,pia ni mwanafunzi wa chuo kikuu Mzumbe kilichopo Morogoro nachukua
Stashahada ya kwanza ya Health Systems Management.Nimemaliza kidato cha nne
katika shule ya St.Francis De Sales na kujiunga na shule ya Loyola High School
ambapo nilihitimu kidato cha sita na kufanikiwa kufaulu vizuri kwenda chuo
kikuu Mzumbe.Katika familia yangu mimi ni mtoto wa pili nikitanguliwa na dada
yangu na mdogo wangu wa kike wa mwisho.
Napenda sana mpira wa miguu ni mchezaji
mzuri na shabiki wa Arsenal FC,pia napenda sana kuskiliza mziki wa dunia nzima
kuanzia hapa nyumbani Tanzania na nchi zingine zote duniani.Napenda sana mziki
wa HipHop na ni shabiki wa Rapper wa kimarekani anaeitwa Fabolous’Loso’ na hapa
nyumbani namkubali Fid Q na Ngwea..R.I.P bro.
Safari
yangu ya mziki nimeanza mwaka 2007 ndipo nilirecord traki ya kwanza iliyoitwa
‘Ishara Ya Ukombozi’ nilikuwa nipo kidato cha pili na nilimshirikisha kaka
yangu wa shule aliitwa ‘Culture’ ambae aliniandikia mistari na produza alikua
Dizzy Mchizy.
Baada ya hapo nikarekodi trak nyingine iliyoitwa ‘Modern Crunk’ na
kuifanyia video iliyopata airtime katika baadhi ya station ikiwemo C2C.Pia
sikuishia hapo,mwaka 2008 nikarekodi nyimbo nyingine iliyoitwa ‘Niache Niongee’
chini ya produza Dizzy Mchizy ambayo kwa namna moja au nyingine ilifanya watu
waanze kunielewa kwamba nina kipaji.Baada ya kufaulu na kuingia kidato cha tano
ndipo nikakutana na Dully Sykes na kufanya nae nyimbo pale Dhahabu Records
iliyoitwa BELIEVE ME mwaka 2010 lakin bahati mbaya nyimbo haikusogea kutokana
na vikwazo mbalimbali ikiwemo shule kunibana.
Mwaka huohuo nikapata idea ya
kufanya mixtape yangu iliyoitwa EL LEGENDEE 1 ambayo ilikua na nyimbo kama
Believe Me,Niache Niongee,Love You,Don’t Go nk.Namshukuru Mungu mixtape watu
waliipenda na kunipa moyo wa kukaza zaidi.Mwaka 2011-2012 ilikuwa ngumu kwa mi
kufanya mzik kutokana na shule kunibana nilikuwa form6 ila nlifanya nymbo ya
‘Sweetlove’ na kuiweka mtandaoni ambayo ilipata downloads zaidi ya elfu3.Baada
ya kumaliza form6 nilifanya video ya nyimbo ‘Imma Getting Em Off’ ambayo
ilitazamwa sana YouTube na kupata sana airtime kwa baadhi ya Station hapa
nchini.
Kwa sasa
nina project ya kufanya Album Yangu itayoitwa ‘The Rise Of The Young Legendee’ na nishafanya baadhi ya
nyimbo ambazo pia zipo kama Trailer katika mitandao mfano HulkShare/yincaskillerflo.Baadhi
ya nyimbo hizo ni kama Sweetlove,Mr A Mill Swag,Show Me.Pia nimetoa Tshirts za
kusapoti hii album ambazo zipo mtaani.Kwa sasa naachia video mbili za nyimbo
zangu SATURDAY na R.I.P.Safari hii nimejipanga vilivyo,am ready for the
competition,,you gotta get stay ready,,watu wangu wasubiri new flavour kwa
industry.
Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipowashukuru hawa watu,,Familia yangu
inayonisapoti,Dizzy Produza,Yuddy,Dully Sykes na wanangu wa
RoyalFAM(makaino,caliross,jose,sonjay,na mtu mzima BigDadi Kimambo)Na watu
wangu wote wanaonisapoti mziki wangu kwa namna moja au nyingine,,,
Nawapenda
sana.
Follow Me
SoundCloud/yincaskillerflo,,,Instagram/yincaskillerflo,,,HulkShare/yincaskillerflo,,YouTube/yincas08…AHSANTE
#Its
Western Musik SwagginUp_RoyalF
No comments:
Post a Comment