World News

Wednesday, July 31, 2013

Kesi ya Jide na Clouds yapigwa Kalenda!

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kinondoni, jana imeiaharisha kesi inayomkabili msanii wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura 'Lady Jaydee' a.k.a Anaconda dhidi ya uongozi wa Clouds Media Group hadi Agosti 2, mwaka huu.


Kesi hiyo ya madai iliyopo mbele ya Hakimu Athumani Nyamlani, jana ilipelekwa kwa ajili ya kusikilizwa lakini ilishindikana kutokana na wakili anayemtetea, Jaydee kutotokea mahakamani hapo na kumtuma mwakilishi wake.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa wakili huyo wa Jaydee, amekwenda katika Mahakama Kuu kuhudhuria kesi nyingine na hivyo kushindwa kufika mahakamani hapo kuendelea na kesi hiyo na hivyo kuahirishwa hadi Agosti 2, mwaka huu.

Kesi hiyo ya madai ilipelekwa mahakamani hapo na Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa Kampuni ya Clouds Media kwa madai ya kuukashifu uongozi huo.
 
 Kwa mujibu wa mdai huyo, ambaye ni uongozi wa Clouds Media ulidai kuwa mdaiwa huyo ambaye ni Lady Jaydee aliandika maneno ya kuukashifu uongozi huo kupitia mitandao ya kijamii.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...