Friday, February 28, 2014

Tetemesha Records Kumtoa UnderGround 'BARAKAH Da PRINCE'


Nachukua fursa hii kumtambulisha msanii mpya wa Tetemesha Records. Anaitwa BARAKA da PRINCE kutoka Mwanza, lakini kwa sasa makazi yake ni Dar ambapo atakuwa hapa moja kwa moja kama makazi yake ya kudumu kikazi.

Amekua chini ya Tetemesha toka mwaka jana lakini kwa kawaida kabla ya kumtoa hadharani msanii mpya hua kuna utaratibu wa ndani katika hatua za kumuandaa ndio sababu ninamtambulisha sasa.

Tegemeeni Video na Audio muda si mrefu kutoka sasa, Video imefanywa na Nisher. Itatangulia kutoka video kisha baada ya wiki itafuata Audio.


Mawasilano ya Barakah:
Simu: 0714 321086

Insta:  @barakah_daprince
Twitter: @barakahdaprince
FB: Barakah da Prince

Kidboy

No comments:

Post a Comment