Tuesday, March 4, 2014

BABY BOY IS BACK!!



Moja kati ya msanii anayefanya muziki wa bongo fleva Edson Wilison a.k.a Baby boy ambaye alipotea kwenye game ya muziki,sasa amerudi kwa kishindo kikali.
Baby boy ambaye alipotea kwa kipindi kirefu, zaidi ya miaka miwili kwenye muziki sasa amerudi na ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Funga Mkanda aliyofanya chini ya studio iliyopo maeneo ya sinza lego jijini dar es salaam inaoitwa Flexible music.
Ngoma hiyo ambayo Baby Boy akiwa amemshirikisha Barnaba boy na  msanii anayeitwa Shazy Melody,ambaye yupo lebo chini ya Flexible Entertainment ikiwa imetengenezwa na  mtayarishaji Basmart  the next hit  wa studio hiyo.
Baby Boy akizungumza kuhusu ujio wake mpya ameeleza kuwa unampa matumaini sana na kuwaomba mashabiki wake wampokee vizuri maana ndiyo amerudi kwa nguvu zote.
“Hii ni ngoma yangu mpya ambayo nimefanya na Barnaba Boy na Shazy Melody na wimbo wangu unaitwa Funga Mkanda ambayo natarajia kuiachia siku yangu ya birthday yaani siku yangu ya kuzaliwa alhamisi ya tarehe 6 mwezi huu” Baby Boy alisema.
Pia aliongeza kuwa ujio wake huo hautaweza kumfanya arudi nyuma tena kwenye muziki na alifafanua kuhusu ngoma hiyo
“Aaah ni ngoma ambayo naelezea jinsi gani nimerudi maana najua mashabiki zangu walikuwa na hamu na mimi kwa kipindi kirefu sana kama mtu aliyekuwa na kiu jangwani”Aliongeza Baby Boy.

No comments:

Post a Comment