Tuesday, August 26, 2014

Wasanii 25 wavamia Bunge la Katiba kuitetea Sheria ya "Haki Miliki" ktk kazi za Sanaa!

Mweyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta (aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasanii walifika Bungeni mjini Dodoma kwa ajili kuwasilisha mapendekezo yao kwajili ya Katiba mpya. Kushoto kwake ni Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Samia Suluhu Hassan. (Picha na Maelezo-Dodoma).




MWENYEKITI wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta amewatoa wasiwasi wasanii wa Tanzania wakati alipokutananao jana Bungeni mjini Dodoma kwalengo la kuwasikiliza wasanii hao wakiwa na kilio chao cha kusahaulika kwa kipengele kinachohusu Haki Miliki (Intellectual Property) za kazi za wasanii katika Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Mhe. Sitta mesema kuwa nidhahiri kuwa Katiba iliyopo sasa imepitwa na wakati kwani haigusii mambo mengine yakiwemo hakiya vitu visivyoshikika kama vile haki hizo za wasanii na wagunduzi hapa nchini.


“Tunachojaribu kufanya hapa Dodoma ni kutunga Katiba ambayo nirafiki kwa kila Mtanzania ili iweze kumsaidia kila mmojakatika eneo lake, hivyo hii itakuwa ni Katiba iliyorafiki”. Alisema Mhe. Sitta.


Aidha, Mhe. Sitta amewapongeza wasanii wote 25 waliowawakilisha wenzao kwakuja Bungeni mjini Dodoma kwaajili ya kuwasilisha mapendekezo yao iliyaweze kutambuliwa kwenye rasimu hiyo.


Wasanii hao ambao wamefuatana na viongozi wao wa msafara, pia amewapongeza kwa kazi kubwa na nzuri waifanyayo wasanii wengi wa Tanzania katika kuitangaza nchi yao.


Naye Mkuu wa msafara wa wasanii hao, ambaye ni Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAF) Bw. Simon Mwakifwamba amemueleza Mhe. Sitta kuwa kuna umuhimu wa Katiba Mpya itakayopatikana ihakikishe inalinda Haki Miliki za wasanii pamoja na utambuzi wakundi kubwa la wasanii ndani ya Katiba hiyo kwani ndiyo wanafanyakazi kubwa ya kuitangaza Tanzania ndani na nje ya mipaka yake.


“Wasanii wanafanya kazi kubwa ya kuitangaza nchi ambapo kwasasa takwimu zamchango wao, katika Pato la Taifa kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2013 ya Chama cha Haki Miliki  cha Kimataifa kwa kipindi  cha mwaka 2007hadi mwaka 2010 sanaa zote imechangia kwa asilimia 4.3% zaidi ya madini, gesi, maji na hoteli, na tasnia ya sanaa imetoa ajira kubwa kwa zaidi ya asilimia 5.6%, hivyo naomba katika Katiba Mpya kuwepo nauungwaji mkono wa wasanii hasa katika kulinda Haki Miliki zao (Intellectual Property).


Kwaupande wake MakamuMwenyekiti wa Bunge hilo,Mhe. Samia Suluhu Hassan  aliwashukuru wasanii hao, kwa kufika Bungeni na kuja na jambo zuri lenye manufaa kwa wasanii na Taifa kwa ujumla na amewahakikishia kuwa maombi yao ya kutaka Katiba Mpya ilinde Haki Miliki za kazi zao ya tafanyiwa kazi.


“Kuja kwenu Dodoma katika shughuli hii kunaonyeesha jinsi mlivyo na upeo , hili ni jambo la msingi kuwekwa katika Rasimu ya Katiba. Huu ni wakati pekee wakuhakikisha mambo yenu yanatambulika,” alisemaMhe. Samia.


Aidha, Mhe. Samia aliongeza kuwa baada ya hapo kinachofuatia ni utungaji wa Sheria kupitia wizara husika.

No comments:

Post a Comment