Mkuu wa Mkoa pichani amewakumbusha wananchi kutokimbilia sehemu za HATARI baada ya maafa yaliyotokea huko Mbagala
Chanzo kikubwa cha ajali hio ya moto ni baada ya 'muhuni mmoja aka msela wa road' kutaka kuiba/kuchomoa betri ya lori la mafuta lililoanguka huku wengine wakiendelea kuiba mafuta ya petroli. Ktk harakati za kuchomoa betri hio kulitokea CHECHE zilizosababisha moto mkubwa wa petroli na kuunguza watu zaidi ya 20
Ajali kama hii imewahi kutokea mkoani Mbeya maeneo ya 'Namba Wani' na watu wengi kupoteza maisha na kuzikwa ktk kaburi la pamoja!
Kumekuwa na kawaida ya baadhi ya watu kutofikiria marambili madhara yatakayotokea baada ya hatari fulani, mara nyingi watu hukimbilia ajali mbaya, milio ya mlipuko navitu km hivyo.
Blogu ya Makavu inaungana na Mkuu wa Mkoa kuwakumbusha wadau kukaa mbali na hatari....
No comments:
Post a Comment