World News

Tuesday, October 28, 2014

Wasanii 'Ruksa' kuvaa Gwanda za Kijeshi!!!

Inasemekana Ras Makunja ndie msanii anayepiga gwanda za kutisha, na sheria ya nchi ya ujerumani inamuruhusu, kwa hizo ajafunja sheria ya bongo


Gwanda za mkuu wa kikosi cha FFU-ughaibuni Kamanda Ras Makunja wa Ngoma Africa band ambaye pia ni mmliki wa himaya ya Viumbe wa ajabu "Anunnaki Empire" yenye makao yake kule Ujerumani,gwanda za mkuu huyo hazina uhusiano wowote na JWTZ,na zoezi linaloendeshwa hapa bongo la kuwasaka wasanii wenye mavazi ya kijeshi ,kamanda Ras Makunja na kikosi chake haliwahusu kwani wao wanaishi nje ya mipaka ya Tanzania,lakini kama ingekuwa wanaishi hapa labda ndio...
Habari zimetonya kuwa mwanamuziki huyo nyota wa kimataifa anayetamba na Bongo Dansi lake kule Ughaibuni Ras Makunja anakijua nini anachokifanya na pia anaheshimu sheria za nchi yake Tanzania kwani gwanda zake uzivalia nje ya mipaka ya Tanzania ,na anapokuja Tanzania kwa likizo yeye ni raia mwema tu vianzo vya habari vimetonya.

mwanamuziki mwingine mwenye gwanda za kutisha katika kikosi cha Ngoma Africa band ni Soloist wa bendi hiyo Christian Bakotessa aka " Afande Chris-B Mshenzi wa solo gitaa" hawa jamaa wanatishaga kule ughaibuni majukwaani wao kuvaa gwanda ni kitu cha kawaida ulaya tena wakisindikizwa na ulinzi wa maaskari wa ulaya ! 
watupie jicho kambini kwao www.ngoma-africa.com

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...