Baadhi ya wawekezaji wa kigeni au pengine watumishi raia wa kigeni wamekuwa wakivunja sheria za nchi kwa kujiingiza au kufanya shughuli zisizo katika miktaba yao ya
kazi,au nje ya vibali vyao vya kufanyakazi hapa nchini Tanzania,lakini
uvunjwaji wa sheria za nchi unaofanywa na wageni hawa unasaidiwa na sisi
wenyewe kwa kuzingatia zile mila zetu na misemo ya ah ! "MGENI WA MUNGU HUYU" mwache ajitafutie riziki.
Matokeo yake tumekuwa na wachoma mahindi mtaani kutoka china,wabeba zege pia, Kumradhi pengine makahaba au changudoa kwenye madangulo ya siri. tunaweza kuwa na wakaanga samaki, walinzi "Kolokoloni" kutoka Thailand na Bangladesh, inawekana kabisa tunao hapa nchini wapishi na tour guider kutoka nchi za ulaya !
Kwa mtindo na utamaduni wetu huu wa ah! wache "WAGENI WA MUNGU " wajitafutie ridhiki tutajikuta tunao akina mama ntilie wakigeni.
Tunajiuliza
wale wawekezaji wanajiusha na biashara za mitumba au maduka ya nguo
kariakoo hivi vibali aliwapa nani? yaani muuza mtumba na duka la sukari
atoke china,Yemen,Bangladesh ulaya ! hii kweli inaingia akilini kwa
watanzania?
Sasa wawekezaji hawa kigeni wanafanya shughuli hizi mcha wa jua kali tena kweupe Mkondo wa sheria ya nchi unavunjwa walinzi wa sheria wako wapi?
Wizara zinazohusika amlioni hili au ndio ah! TUWAACHE WAGENI WA MUNGU wajitafutie ridhiki ? Watanzania ukarimu ni jadi yetu ! misemo hii haifanani kabisa na ukiwikaji wa sheria za uhamiaji na ajira za nchi, kwani katu kwame huruma na haki havikai pamoja.
Serikali iangalie hawa wawekezaji!! Wanatubania nafasi zetu bureeeeee
No comments:
Post a Comment