World News

Tuesday, November 11, 2014

Vita Wamasai na Wamang'ati yanukia Kisaki Morogoro!

Siku ya jana jioni ktk Kata ya Kisaki kwenye kituo cha Polisi huko Morogoro kulizuka tafrani kati ya Wamasai na Wamang'ati juu ya ugomvi wao wa mifugo, Wamang'ati wakiomba ruhusa kutoka jeshi la Polisi wawachape hao wamasai mpaka watakaporudisha ng'ombe zao 50.

Inasemekana kuna kijana wa kimasai aliiba(alionekana akiziswaga) ngombe 50 kutoka kwa wamang'ati, nao wamang'ati wakaungana na wasukuma na wakurya wakaamua kuvamia kwa wamasai na kuswaga ng'ombe zao mpaka ktk kituo cha Polisi huku wakizishikiria mpaka wamasai watakaporudisha za kwao.

Mpaka naondoka eneo la tukio Wamang'ati, wasukuma na wakurya waliungana kutaka kuwatandika Wamasai.

Wamang'ati ni mafundi sana wakutumia mishale, wakati wamasai wao hutumia mikuki zaidi......... hakika km Serikali itawaacha hawa jamaa wadundane, maafa ya Kilosa yatajirudia Kisaki

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...