Kanisa lisilo rasmi la mchungaji Mchungaji Josephat Gwajima
lililokuwa likiendesha shughuli zake kinyume na taratibu katika viwanja
vya Tanganyika Packers Kawe,wilaya ya Kinondoni,jiji Dar limeamriwa
kuondoka mara moja na kuwacha eneo hilo wazi kwa ajili ya maendeleo ya
watu wa kawe.
Kanisa hilo ambalo kwa muda mrefu limekuwa likiendesha
shughuli zake kinyume na taratibu na kusababisha usumbufu na kero kubwa
za makelele kwa wakazi wa maeneo hayo.
Katika Barua iliosainiwa na
Meneja wa Mkoa wa Kinondoni wa shirika la nyumba la Taifa imesisitiza
kwamba pamoja na kutambuliwa umuhimu wa kanisa hilo kuendesha shughuli
zake lakini shirika hilo halitaweza kutoa ruhusa kwa kanisa hilo
kuendelea kufanya mahubiri katika viwanja hivyo,kwani shirika hilo
limeshaanza kutumia Viwanja hivyo kwa maendeleo ya wananchi wa KAWE
ikiwa ni ujenzi wa makazi n.k
Bw Masika ametoa siku 30 tu ili
Mchungaji Gwajima kujitayarisha na kuwacha viwanja hivyo wazi kwa ajili
ya maendeleo ya wananchi.
No comments:
Post a Comment