World News

Tuesday, March 31, 2015

PUMZIKA KWA AMANI 'ABDUL BONGE'

MWILI wa aliyekuwa mwanzilishi wa kundi la Tip Top Connection, Abdul TaleTale (Abdu Bonge), unatarajiwa kuzikwa leo kijijini kwao Mkuyuni mkoani Morogoro.

Abdul Bonge anadaiwa alifikwa na umauti Machi 28 alipokuwa akikimbizwa katika Hospitali ya Mwananyamala muda mfupi baada ya kusukumwa na kuanguka alipokuwa akiamulia ugomvi wa vijana karibu na nyumbani kwao Magomeni, Kagera.

Wasanii mbalimbali waliowahi kufanyakazi na Abdu Bonge enzi za uhai wake walimsifia kuwa na moyo wa kuendeleza muziki hasa wa kizazi kipya na pia alikuwa msikivu kwa wasanii hata kipindi alichoamua kumuachia shughuli zote za usimamizi wa wasanii mdogo wake, Babu Tale.
Marehemu Abdul Bonge atakumbukwa kwa kazi yake nzuri ya kuwaibua wasanii mbalimbali wa muziki wa Bongo Fleva wakiwemo Madee, MB Dog, PNC, Pingu na Deso, Keysha, Tunda Man na Z Anto.


MBELE YAKO NYUMA YETU.....PUMZIKA KWA AMANI KAKA!!

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...