Tokyo,Japan,
Wanamuziki
wa kongwe wa muziki wadansi Abbu Omar Njenga aka Abbu Omar na Fresh
Jumbe Mkuu wenye ngome yao nchini Japan,siku ya jumamosi 21 Machi 2015
walitia fora kwa kushiriki jukwaani na kumpa baraka zote mwanamuziki
Ally Choki katika onyesho lililofanyika katika ukumbi wa Sonudai-Kanagawa Prefecture, Sagamihara City,Tokyo ,Japan.
Wakongwe hao waliobobea katika muziki kwa maiaka mingi Abbu Omar Njenga mpiga gitaa au mpini na mtunzi aliyewahi kutamba na bendi za UDA JAZZ na mwaka 1981 alijiunga na Simba wa Nyika nchini Kenya na hatimaye kujikita nchini Japan kwa miaka mingi na mwenziwe mkongwe Fresh Jumbe Mkuu aliewahi kuwa mwimbaji mtunzi wa bendi za Dar International (Super Bomboka),DDC Mlimani Park "Sikinde na pia Juwata Jazz band aka Msondo Ngoma ,wakongwe hawa ni mfano wa kuigwa pamoja na kuwa wameliteka soko la muziki wa kiafrika nchini japani na kungineko lakini wapo mstari wa mbele kuwaunga mkono na kuhakikisha kuwa wanamuziki wa nyumbani Tanzania waingiapo Japan wanateka soko.
No comments:
Post a Comment