World News

Thursday, May 28, 2015

Madai ya Watoto wa B.B KING 'Patty na Karen' kuwa baba yao aliuwawa kwa sumu......ni kupagawa baada ya kuachiwa urithi wa $5,000/= tu! - Mwanasheria.


Watoto wa kike Patty King na Karen William (pichani) wa Mwanamuziki mkongwe aliyefariki wiki mbili zilizopita Marekani B B KING, wamedai baba yao aliuwawa kwa sumu, madai ambayo mwanasheria wa mzee wao amekanusha na kusema hiyo yote ni mshtuko kutokana na kutegemea kuachiwa mkwanja mrefu tofauti na ukweli wenyewe wa MIRATHI ambapo kila mtoto kaachiwa dola 5,000 na wajukuu dola 3,000.

“My guess is the children and grandchildren don’t like the fact he’s leaving them $3,000 and $5,000 each and then leaving the rest to his lineage for education,” lawyer Brent Bryson told the Daily News. “B.B. did not have a very high formal education, and he wanted to have his lineage go to college, so he set up a trust that would pay for college and other expenses.”

B B KING mkali wa blues na kupiga guitar aliyewahi kujinyakulia Tuzo 13 za Grammy huko Marekani, ameacha watoto 15 kutoka kwa wanawake 15 tofauti amefariki akiwa na umri wa miaka 89.

Mwanamke pekee aliyekuwa akimuhusudu na kumpenda kwa dhati ni Gitaa lake alilolipa jina la Lucile.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...