World News

Wednesday, June 3, 2015

NGOMA AFRICA BAND AKA FFU WALIFUNIKA


Bremen,Ujerumani,
Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa Band aka FFU-Ughaibuni wanazidi kudatisha ughaibuni !

Katika onyesho lao ndani ya hekalu la Uebersee Museum mjini Bremen,ujerumani usiku wa jumamosi 30 Mei 2015 bendi imeonyesha kwa kiasi kikubwa kuwa inakubalika katika hadi katika mahekalu ya kutisha,Kikosi kazi hiko maarufu kwa muziki wa dansi barani ulaya kinachoongozwa na mwanamuziki kamanda Ras Makunja,kikiwa na wanamuziki waliojaa vipaji akiwemo yule mcharaza gitaa machachali Chris-Bakotessa aka Afande Chris-B,wanazidi kuongeza kasi ya kupenya kila kona na kufunika,na kuifanya bendi hiyo kuwa bendi ya kwanza ya kigeni kuwa tishio barani ulaya.
 
 
Ngoma Africa band inayodumu katika medani ya muziki kwa muda wa miaka 22 imegeuka kuwa muzimu wa muziki wenye mvuto wa ajabu na mdundo wao wa "Bongo Dansi". 
 

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...