World News

Wednesday, August 19, 2015

Kupitia Kauli ya Dkt. Magufuli, Lowassa afananishwa na Rais Ronald Reagan wa USA aliyekuwaga mdau wa Sanaa!

Raisi wa 40 wa Marekani Ronald Wilson Reagan aliyetawala kwa vipindi viwili kati ya mwaka 1981 mpaka 1989


Ktk kikao cha uvccm Dsm, 
Dk Magufuli alisema baadhi ya wapinzani ni waigizaji wakubwa ambao wamesomea uigizaji na wataufanya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu kutawaliwa na mbwembwe na maigizo mengi.
Alisema kazi kubwa ya CCM ni kukabiliana na mbwembwe na maigizo hayo ili kuyashinda.
Magufuli alisema CCM siyo watu wa matumaini, bali ni watu wa maendeleo na safari ya uhakika.
Alisema wapinzani wa CCM sasa wameanza kunukuu kila kitu hasa nyimbo za chama.
Aliwaambia vijana hao: “Katika mchakato huu na katika uchaguzi wa mwaka huu kuna mbwembwe nyingi, kuna mbinu nyingi na kuna maigizo mengi hasa kwa sababu wako wengine walisomea maigizo. Kwa hiyo tuna wajibu wa pamoja kuyashinda haya maigizo.”

CHANZO: Mwananchi 17 .08. 2015


Japokuwa hakutajwa jina Kitaaluma Mh. Lowassa ana shahada ya kwanza ya SANAA na ELIMU BA (Edu) Hons kutoka UDSM na ya pili ya Masters ya Maendeleo ya Jamii kutoka Chuo kikuu cha Hull Uingereza.

Hivyo wadau wamemfananisha Lowassa na aliyekuwa Rais wa Marekani Ronald Reagan aliyeliongoza taifa lake kwa mafanikio licha ya kuwa na taaluma ya  Sanaa 

1 comment:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...