World News

Monday, August 17, 2015

MASHINDANO YA UREMBO TANZANIA YAFUNGULIWA TENA!!

Mkurugenzi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari leo wakati wa kutangaza kuifungulia kampuni ya Lino International Agency kuendesha shindano la Miss Tanzania. Kushoto ni Mkurugenzi wa Lino, Hashim Lundenga.

Awali Serikali ya Tanzania iliyafungia kwa miaka miwili mashindano ya Miss Tanzania baada ya waandalizi kudaiwa kukiuka taratibu na kanuni.

Mashindano hayo yaliofunguliwa mwaka 1994 yamedaiwa kuwa na upendeleo mbali na rushwa kulingana na malalamishi yaliotolewa na wananchi pamoja na washiriki.

Kwa mujibu wa kaimu katibu mtendaji wa Baraza la Sanaa nchini Tanzania Basata , Godfrey Mngereza,kamati ya miss Tanzania ilikiuka kanuni na taratibu zinazoongoza mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...