Kupitia mtandao wake wa kijamii msanii wa Hiphop Tz Nikki Mbishi Baba Malcom ametoa yake ya moyoni juu ya muziki wa Tz
Mawazo/Maoni Yangu:
Obviously kwa utafiti wangu mdogo naweza kusema
muziki wetu wa Tz unakufa gradually na wale wanaojiita wadau wanajua
hilo ila kwa kuwa washachukua vyao mapema na watu wao basi hakuna namna
zaidi kufunga na kufanya maombi tu.
Muziki umekuwa kama kitu cha
kifamilia,yaani kama sio mwanafamilia kupata nafasi kwenye nyanja yoyote
itabaki ndoto kwenye career yako hata uwe una uwezo wa Nabii Mussa.
Huwa najiuliza hivi,kama wadau wameweza kuwabrand wasanii watano Tz
nzima wakafika hatua fulani kisanaa,kwanini wanashindwa kubrand wasanii
100 ambapo uwezo huo wanao kupitia patnerships zao walizonazo na
makampuni makubwa.
Tz imelaaniwa kwenye sekta ya sanaa,michezo na burudani wanaojiita wadau hawana hata aibu kujifanya wanajivunia mafanikio.
Msanii gani Tz amesainiwa na Label kubwa Duniani ukimtoa Rose Mhando?
Tz ni kujuana kwingi kuliko kuweka professions mbele,kila fursa
inatumika kunufaisha wachache na kukandamiza wengi,kitu kinachopelelea
hata baadhi ya wanahiphop wanaojiita wanaharakati kuwa WANAFIKI wa
kutupa wakiofia watapotezwa kwenye game au kukosa vijisenti vya wao
kutamba mjini na mnawajua hao watu.
Msanii mwenye recognition na
reputation kubwa anatengeneza project nzuri ambayo ni feasible na
reasonable,anakwenda kupropose for sponsorship kwenye kampuni fulani
anazungushwa mpaka anajuta kuwa msanii ili hali tunawafahamu watu ambao
hata wakiandaa show vichochoroni wanadhaminiwa na makampuni makubwa
licha ya ubovu wa contents zao.
Itaendelea....
https://www.facebook.com/nikki.babamalcom?fref=n
No comments:
Post a Comment