Saturday, June 27, 2009

Aliyeuawa kinyama Sio OMMY G wa hit song 'Kindumbwendumbwe' tunayemjua !!



Gazeti la Sani lililotoka kwenye tarehe 24 wiki hii lilikua na habari kwenye back page yake iliyokua inasema "OMMY G AUAWA KINYAMA". Wadau wengi walipatwa na mshangao na kupiga simu kuuliza kulikoni, mchizi amedead au!!


Ukweli ni kuwa Aliyeuawa sio Ommy G Gansta aliyetoka na ngoma ya 'Kindumbwendubwe' akishirikiana na Nalenale pamoja na Pig Black dude lililotengenezwa na Mika Mwamba 2001.

Ommy G

Km gazeti la Sani lilivyoripoti jamaa aliyeuawa kinyama anaitwa Hamidu alikuwa ni msanii pia na jina la kisanii pia alijiita Ommy G huko pande za Tanga na aliuawa kikatili na kutupwa mtaloni na watu wasioeleweka mpaka hivi sasa wakati anatoka kwenye burudani usiku.

Dullayo a.k.a D timing

Ommy G a.k.a Gansta a.ka Vampire baada ya Kindumbwendubwe aliachia nyimbo zingine km Choo cha kike, Rudi mwana, Hiphop imenoga na Sikiza mchumba ambayo ni mpya kwa sasa na rafiki yake mkubwa ambae wapo kwenye familia 1 ya makavu ana album sokoni inayoitwa IMANI, na pia yuko mbioni kutambulisha single mpya inayoitwa Naumia Roho, wote wanaskika kwenye nyimbo ya 'Ongea mwana' na 'Maneno'.

Wakati haya yanatokea huku, Ommy G na Dullayo wapo Iringa town ambapo usiku wa kuamkia leo walikua na mwaliko wa show ktk ukumbi wa Mkwawa university na kwa taarifa zilizopatikana show ilimalizika salama salimini, wamepiga show kali sambamba na kutambulisha nyimbo zao mpya pamoja na zile za familia ya Makavu-live Ongea mwana na Maneno wapi ambayo ipo ktk maadhi ya mchiriku.

No comments:

Post a Comment