Miss Dar City Center mpya Slyvia Shali (katikati) akiwa ktk picha ya pamoja na mshindi wa2, Gladis Shao (kushoto) na wa3, Anne Moses baada ya kuutwaa umalikia wa kitongoji hicho.
Mrembo Sylvia Shali usiku wa kuamkia jana alitwaa umalkia wa kituo cha Dar City Center baada ya kuwashinda wenzake 13, katika kinyang'anyiro kilichofanyika kwenye viwanja wa hoteli ya Lamada, Ilala jijini Dar es Salaam.
Kutokana na ushindi huo, Sylvia alipata nafasi ya kushiriki Miss Ilala mwaka huu na kuzawadiwa kitita cha sh. milioni moja kutoka kwa waandaaji wa mashindano hayo Kampuni ya Sisi Entertainment.
Mshindi wa pili alikuwa Gradis Shao ambaye pia alipata nafasi ya kushiriki Miss Ilala na kitita cha sh. 600,000 wakati Anne Moses aliyekuwa wa tatu aliondoka na sh. 400,00 na pia kushiriki Miss Ilala.
No comments:
Post a Comment