Thursday, June 25, 2009

' AY ' KUFANYA SHOW YA KUWACHANGIA WATOTO WASIOJIWEZA JUNI 27 MZIZIMA DSM


Msanii wa kizazi kipya Ambwene Yesaya 'AY' anatarajia kutoa burudani anayoiita "Summer Fiesta 2009" kwaajili ya kuchangia watoto wasiojiweza itakayofanyika Juni 27 mwaka huu katika shule ya sekondari Mzizima, Dar es Salaam. AY amesema, amejiandaa vizuri kutoa show kali kwa ajili ya kuchangia watoto hao ambao hawajiwezi.


Kutokana na tatizo hilo kushamiri kwa watoto hapa nchini limemgusa sana hivyo amewataka watu kujitokeza ili kuweza kuwachangia watoto hao ili kuweza kupata haki zao za msingi.


Pia AY anatarajia kutoa burudani Juni 26 mwaka huu mjini Tanga katika ukumbi wa Club ya La Cassa Chica akishirikiana na mwanamuziki Nonini kutoka nchini kenya. Burudani hiyo itakuwa ni maalumu kwa wakazi wa mkoa huo ambayo imeandaliwa na kampuni ya Maji Marefu Entertainment ambapo mwishoni mwa mwezi Julai AY anatarajia kwenda Poland, Djibouti na Malaysia kwa mialiko kwa ajili ya kutoa burudani.

No comments:

Post a Comment