Mchuano wa kumsaka malkia wa Vodacom Miss Dar City Centre 2009, unatarajia kufanyika kesho katika hoteli ya Lamada, ambapo mshindi wake atatunukiwa taji la litongoji hicho na kupata nafasi ya kushiriki mashindano ya kanda ya Kinondoni.Washiriki wa mashindano hayo, ambao wameweza kushiriki kazi mbalimbali za jamii za kusaidia waathirika wa mabomu Mbagala, kupima UKIMWI na kutembelea mitambo ya kusukuma maji ya Kampuni ya DAWASCO ya Ruvu chini iliyoko wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Sisi Entertainment, John Dotto, alisema wasichana wanaowania taji hilo tayari wamejifua namna ya kunengua jukwaani kwa kufundishwa na msanii mahiri wa bendi ya muziki wa dansi ya African Stars, 'Twanga Pepeta' Hassan 'Super' Nyamwela."Tayari Super Nyamwela, amejiridhisha na kwamba wanyange hao wanafanya vyema hivyo mashindano hayo yatakuwa na mvuto wa aina ya kipekee, yawezekana yakawa na taswira ya Miss Tanzania kutokana na maandalizi ya nguvu tuliyofanya,”.
Licha ya burudani hiyo, washiriki wa kinyanga'nyiro hicho nao watakuwa na kazi pevu ya kutoa shoo waliyojifunza kutoka kwa Super Nyamwela.Wanyange wanaotarajiwa kujimwaga jukwaani kesho kusaka umalkia wa kitongoji hicho ni Gladys Shao, Anne Moses, Debra Thomas, Sylvia Shally, Brenda Aloyce, Elizabeth Ernest, Jovina Michael, Magreth Peter, Fatuma Bongi, Mwantumu Rajabu, Christine Ivan, Ema Gasule na Neema Mashala.
Mashindano hayo yanadhaminiwa na Vodacom Tanzania , Redds, Yellow Pages, CDS, Syscorp Media, Global Publishers, La-Fiesta Pub, ANGAZA ZIDI, Mombasa Raha, CXC Afrika, Fredito Entetainment, Masoko Agency, Lamada hoteli, Mwasu Fashion na mwanamitindo Fatuma Amour.
No comments:
Post a Comment