Baada ya vipindi vitatu vya lile shindano kubwa la kuvutia la Big Brother Africa, sasa maandalizi ya BBA IV yameshaanza. Imetangazwa mfululizo wa vile vipindi kwenye Tv itaanza kuonyeshwa mwezi September shindano linapoanza ambapo hili la sasaivi litakua maradufu zaidi ya yaliyopita, BBA IV its THE REVOLUTION.
Zawadi kwa mshindi imezidishwa mara mbili zaidi ya ile ya awali ambayo ilikua dola za Marekani 100,000. Mara hii ya nne waandaaji kupitia kituo cha M-net wamefanya mabadiliko makubwa kama nyongeza kubwa ya zawadi, pia kutakua na camera 40 na vipaza sauti 100 kwenye jumba.
Nchi shiriki zimeshaanza kutafuta wawakilishi wao, hapa Tanzania mshiriki atatafutwa kwa siku mbili juni 17 na 19 katika hotel ya Movenpick, jijini D'Salaam.
Mshiriki anatakiwa kuwa na umri zaidi ya miaka 21, awe raia mwenye ufahamu wa Kiingereza na hati ' passport ' ya kusafiria. Mchujo utaanza saa 2 asubuhi mpaka saa 1 jioni.
Tanzania imewahi kutoa mshindi wa BBA2 Richard huku aliyemtangulia Mwisho Mwampamba akishika nafasi ya pili BBA1, Mwaka jana msichana wa kwanza kuwakilisha Tanzania katika mashindano hayo Latoya hakufanya vizuri.
mshiriki wa bba1 Mwisho wa Tz
mshiriki wa bba3 Latoya wa Tz
No comments:
Post a Comment