Kundi la mziki wa bongofleva Tmk Wanaume Family lenye maskani yake Temeke,DSM limetunga na kuutoa wimbo maalum unaozungumzia janga la mabomu yaliolikumba jiji la D'salaam hususan wakazi wa Mbagala.
Wimbo huo ulioimbwa kwa huzuni kufuatia mada yenyewe umetengenezwa ktk studio ya Sound crafterz iliyoko Temeke jijini DSM. Mkubwa Fella alisema wimbo huo unaoitwa " Hili Tatizo " unawaliwaza waale walioathirika na milipuko ya mabomu sambamba na kutoa wito kwa watanzania na wakazi wa jijini kuwasaidia kwa hali na mali waathirika wa ajali hio.
Wadau, TMK wameliona kuwa hili ni janga na ni tatizo hivyo wametengeneza wimbo kutukumbusha watanzania umuhimu wa kuwasaidia ndugu zetu walioathirika na majanga haya.
Pia Juzi kwenye tamasha la TUSIMAME PAMOJA la kuwachangia waathirika wa mabomu Mbagala TMK Wanaume walishiriki vyema na kukonga roho za wapenzi wa muziki waliohudhuria kusapoti mshikamano huo. "Jamaa waliwaamsha watu kutoka jukwaani kuja chini uwanjani kucheza ile staili ya mapanga Dar mpaka Moro".
No comments:
Post a Comment