Kampuni ya Bongo 5 Media Group kuanzisha tuzo kwa wanamichezo pamoja na wasanii ambao watakuwa wamefanya mambo makubwa katika kazi zao ikiwa moja ya kuthamini mchango wao katika jamii.
Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Lucas Naghest alisema zoezi hilo linatarajia kuanza hivi karibuni na tuzo hizo zitatambulika kama “ Tuzo za Watu” ambazo zitahusisha watu wote hasa wanamichezo na wasanii.
Lengo la tuzo hizo ni kuwapa hamasa wasanii pamoja na wanamichzeo ambao wamekuwa na mchango mkubwa katika jamii lakini hawajapata faida kupitia kazi zao.
Alisema tuzo hizo zitawagusa watu wa aina mbalimbali kutokana na kazi yao na tuzo hizo zitakuwa ni nyimbo bora, mwimbaji bora wa kiume na kike, mwanamichezo bora, mwanasiasa, sinema bora, mcheza filamu bora wa kiume na kike pamoja na wengine wengi.
Washindi wa tuzo hizo watapatikana kwa njia ya ujumbe mfupi kupitia simu za mkononi, barua pepe pamoja na tovuti ya tuzo ya watu ambapo itatoa fulsa kwa mtu kumchagua anayestahili kuwa mshindi wa tuzo husika.
No comments:
Post a Comment