Ubeti wa kwanza;
Naomba uniweke ndani ya chupa ili kwako nifike kabisa Mchumba nichizike,nife, nizikwe na wewe kabisa Binadamu.. ME... nafahamu sijakamilika niponde kama Wadau wa ZE UTAMU kila dakika nitafurahi kama utanimwaga, nikija kwa gia za mkwanja nitarudi kujipanga kiunderground kama Alphanga/ 'NAAHIDI' kukupa moyo ukinifanya niwe na wivu, kwa mfano nikituma meseji naomba uchelewe kunijibu ' na sio lazima' kila sehemu ninayokualika utokee, au kila simu ninayokupigia ewe Malkia uipokee nyingine unaweza zichunia hiyo inaweza saidiakuniweka roho juu na kunijaza uchungu pia tusikutane leo mtaani halafu kesho eti uibuke ghetto nizungushe ili nijitoe mwisho wa siku niingie mpeku usinikubali haraka sababu utaharibu mapenzi nami sitaki kukuacha au tuishie 'ONE NIGHT STAND'sijakupenda leo tu kwa sababu tumekutana nilikupenda long time hadi hii leo nakupenda sana nikikutazama napata hisia za kuoana sio kukudanganya kisha nikaishia kukuoa
KIITIKIO:
'NISUMBUE SUMBUE, USINIKUBALI HARAKA HARAKA MIMI' MIE SITAKI KUKUACHA, LOVE NAOMBA UJIAMINI..
Ubeti wa pili:
Usiniambie rangi uipendayo acha mwenyewe niitafute/ 'usitunze' kila zawadi ninayokupa nyingine zitupe ili nijifunze ninapoingia ndani ya duka bei isishuke 'usijichubue' kwakuwa wanazusha eti napenda ngozi nyeupe niimbie usiulize ya rado tu, mkere FIDQ ukiona hainiumizi bado ujue kwako nimefika FULL nimechizika BOO, sio kama ninapita tu/ sijajipachika kama STICKR nimekita kama TATTOO 'KAMA UNANIPENDA NIPENDE' lakini usinikubali haraka, we ni jangwa mie ni mtende nimekuja kama sadaka wote walionikubali haraka hatukudumu tuliachana sitaki kuamini nina zali eti kwakuwa ninajulikana sijakupenda leo tu kwakuwa tumekutana, nilikupenda long time hadi hii leo nakupenda sana nikikutazama napata hisia za kuoa na sio kukudanganya kisha nikaishia kukuoa.
KIITIKIO:
'NISUMBUE SUMBUE, USINIKUBALI HARAKA HARAKA MIMI' MIE SITAKI KUKUACHA, LOVE NAOMBA UJIAMINI..
No comments:
Post a Comment